KWA WENYE KAMPUNI (WAKURUGENZI NA MAKATIBU WA KAMPUNI)

KWA WENYE KAMPUNI (WAKURUGENZI NA MAKATIBU WA KAMPUNI)

Bexb

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2016
Posts
715
Reaction score
1,619
Habari ya wakati huu wakuu. Nimerudi tena ili tuweze kukumbushana baadhi ya mambo ambayo ni muhimu katika uendeshaji wa kampuni zetu
Kufikia leo tarehe 4 mei tumebakiwa na takribani siku 57 kuwasilisha ritani ya mahesabu ya mwaka ya kampuni yaani Annual Audited Financial Statement ambayo ukomo wake wa uwasilishaji ni tarehe 31 juni, 2024 kwa kampuni zilizoingia ama zilizokuwepo sokoni kwa mwaka wa kodi 2023 ambao ulianza mwezi Januari 2023 na kumalizika mwezi Desemba 2023.
Hivyo basi nikukumbushe kuwa hili ni takwa la sheria za kodi na endapo utashindwa kulitekeleza utakutana na adhabu za fine kutoka TRA.
Jitahidi kupata muhasibu wako mapema aweze kukuandalia hesabu hizo ili kuepuka na kero ya kuwasilisha mwishoni kwani wahasibu wengi hupandisha gharama zao na pia wakati mwingine huweza kutokea changamoto ya mtandao.
 
Ushauri kwa wale waliosajili kampuni mpya kuanzia mwezi juni 2023 na unaona kuwa hali yako ya kiuchumi haikuruhusu kufanya hayo mahesabu ama hujaanza biashara ama hukufanya biashara kwa mwaka 2023 basi nashauri uweze kuandika barua kwenda ofisi yako ya TRA kuwaomba kuwa unatarajia kuwasilisha hesabu za miezi kadhaa ya mwaka 2023 kwa pamoja na mahesabu ya mwaka 2024 kwa pamoja.
Hakikisha tunafuatilia majibu na ukijibuwa basi utakua salama na utaokoa gharama za kutafuta auditor kwa ajili ya kazi hii.

Asante.
 
Wachangiaji hapa lazma wawe wachache sana..ila napenda sana kujifunza ukipata mda shusha vitu
 
Hapo nyuma niliwahi kuwa naandika sana kuhusu haya masuala kwa ID nyingine lakini nikaona haya mambo yamekosa wadau nikapotezea. Acha nirudi kwa nguvu sasa.
Wachangiaji hapa lazma wawe wachache sana..ila napenda sana kujifunza ukipata mda shusha vitu
 
Back
Top Bottom