Kwa wenye uzoefu na mafundi jokofu naomba msaada

Magere Cheops

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
213
Reaction score
306
Habari ndugu zangu,

Naomba msaada na ushauri kuhusiana na hii freezer yangu.

Nilinunua mpya dukani hapo Katoro kwenye maduka ya vifaa vya umeme ni kampuni ya Hisense ina ujazo lita 100.

Nimetumia kwa muda wa wiki tatu, ingawa wiki ya kwanza haikuwa na changamoto ila kwa hizi wiki mbili imekuwa na shida hizi.

1: Inachukua muda mrefu sana kugandisha barafu (zaidi ya masaa 48) sijui kama ni kawaida maana sijawahi kutumia.

2: Inapiga short sasa kila unapoigusa ikiwa imechomekwa kwenye socket haijalishi kuna umeme au hakuna umeme.

Naomba kwa anayefahamu tatizo au mzoefu anisaidie hapa.

Je, inawezakuwa na tatizo gani waungwana

IMG-20221120-WA0011.jpg

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Duuh watu wa Katoro mmetisha sana, hapo ni huenda gesi imepungua katika kipindi cha usafirishaji na suala ka kupiga shoti hilo ni tatizo la kukosa earth haipo sawa sawa kuna ulazima wa kuangaliwa mfumo huo kwenye hiyo nyumba.

Watafute mafundi waje wakuangalizie gesi au kama ina warranty irudishe dukani na fundi umeme aje kama nilivyokueleza hapo juu.
 
Kwa uzoefu nilionao, bidhaa za hisense ni kimeo mbaya, nina ushahidi wa kwangu binafsi, mdogo wangu na marafiiki ongeza na ww.

Kibaya zaidi hazitengenezeki zikatulia. Ushauri, tafuta friji nyingine tena nunua hizi hizi zinazoonekana yebo yebo boss zinakaa.
 
Hii inaweza kuwa kweli maana imesafiri kutoka katoro mpaka Kibondo na usafiri wenyewe wa kuungaunga

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Kwa uzoefu nilionao, bidhaa za hisense ni kimeo mbaya, nina ushahidi wa kwangu binafsi, mdogo wangu na marafiiki ongeza na ww.

Kibaya zaidi hazitengenezeki zikatulia. Ushauri, tafuta friji nyingine tena nunua hizi hizi zinazoonekana yebo yebo boss zinakaa.
Duuuh.....kununua nyingine labda mpaka mwakani sasa....ila wanavyojinadi sasa hawa Hisense kwamba bidhaa zao ni bora na ghari mpaka kerooo

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Kwa uzoefu nilionao, bidhaa za hisense ni kimeo mbaya, nina ushahidi wa kwangu binafsi, mdogo wangu na marafiiki ongeza na ww.

Kibaya zaidi hazitengenezeki zikatulia. Ushauri, tafuta friji nyingine tena nunua hizi hizi zinazoonekana yebo yebo boss zinakaa.
Mimi ninayo ina miezi mitano, ikigandisha, hata umeme ukatike, barafu inakaa zaidi ya masaa 24 ndio inaanza kuyeyuka.
Siku ikianza kuzingua nitaleta mrejesho.
 
Back
Top Bottom