Kwa wenye uzoefu na mikopo ya benk/sheria za mikataba

m2me

Member
Joined
Jul 23, 2012
Posts
63
Reaction score
16
Habari zenu wadau,
Kwanza niwapongeze waliobuni na kuanzisha jukwaa hili ambalo siyo tu ni chanzo cha habari mpya, burudani bali pia kisima cha maarifa. Hapana shaka kuwa kila anayetembelea jukwaa hili huondoka na fikra na mtazamo tofauti juu ya maisha yake binafsi, taifa na mahusiano yetu kimataifa.

Kwa kutambua hilo, nimeona nitake msaada wa kisheria hasa sheria za mikataba na fedha. Nilichukua mkopo kutoka benki moja hapa nchini tawi la Mwanza kwa dhamana ya mwajiri wangu kwa makubaliano ya kukatwa kiasi fulani cha fedha kutoka kwenye mshahara wangu kwa kipindi cha miaka 3 ambapo natarajia kumalizana nao ifikapo October 2015.

Pamoja na makubaliano hayo, na kama mnavyojua hizi asasi zinazotegemea wafadhiri kwa asilimia 100, hatuna mishahara kwa zaidi ya miezi 6 sasa japo kuna matumaini kuwa hali inaweza kutengamaa kuanzia mwezi ujao (Octoba).
Kutokana na hali hiyo, nimeshindwa kabisa kurejesha kiasi chochote kwa zaidi ya miezi 6 kutokana na ukweli kuwa mkopo huo nilijaribu kuingiza kwenye biashara nikakutana na changamoto kadhaa ikiwemo ajali na wizi.

Baada ya kuona kimya "hakuna marejesho kwa miezi kadhaa" zikaanza simu zinazojitambulisha kuwa ni kutoka makao makuu ya Bank husika, zikifuatilia mkopo huo ambapo nilijaribu kuwaeleza hali halisi ya mishahara kwani ndo iliyokuwa nyenzo pekee ya ulipaji wa deni hilo.

Simu hazikukoma lakini pia afisa mfuatiliaji wa mikopo kutoka tawi la benk hiyo alifika ofisini kwetu na kuzungumza na mwajiri ambaye alimweleza hali halisi kuwa tupo (hatujaacha kazi) ila mishahara ndo hakuna kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu.
Pamoja na majibu hayo kutoka kwa mwajiri na ukweli kuwa tulishapewa barua zinazoeleza hali ya uchumi wa ofisi yetu na kuruhusiwa kutafuta kazi kwingine au kuendelea kuvumilia hadi hali itakapotengamaa, bado simu zimeendelea kupigwa na safari hii deni langu likizidishwa kwa zaidi ya mara tatu ya deni halisi.

Hali hiyo ilinishtua na hata kulazimika kutembelea tawi la benki hiyo ambapo afisa mikopo alinieleza kuwa wanaopiga simu ni madalali waliopewa jukumu la kufuatilia deni hilo na kuwa hawataacha kunipigia simu kwani wanatimiza kipengele chao kabla ya hatua itakayofuata ya kukabidhiwa kwa mfilisi ambaye atakapo ingia kazini atakamata hadi simu ya mchina ninayotumia.

Pia alinieleza kuwa kiasi ninachotajiwa na dalali siyo cha kweli ila kinaweza kufika hapo baadae kama sitolipa deni hilo mapema kutokana na adhabu "fine/penalty". Dalali anasema deni langu ni milioni 7, Benki wanasema million 3.6 na mimi natambua deni la milioni 2.2

Msaada:
1. Ni kwanini kuwe na adhabu wakati benk inafahamu kuwa kwa sasa sina mshahara na dhamana yangu ni mshahara?
2. Kwa nini adhabu hiyo isianze kutumika baada ya tarehe ya mwisho ya urejeshaji mkopo (Oct, 2015)? Kwani katika kipindi hiki harakati ninazofanya zinaweza kuzaa matunda na hata nikaweza kurejesha kiasi chote (2.2 m) hata kabla ya tarehe hiyo.
3. Mwajiri anawajibika vipi na deni hilo? Au nini msaada wake kisheria?
4. Je, ni sawa kisheria benk kupiga mnada mali za familia kama shamba, nyumba/gari amabavyo nimevipata nje ya mkopo huo?
5. Je, ni sahihi benk kuendelea kunipiga ‘fine' hata baada ya kuonesha nia ya kurejesha kidogo kidogo kwa kadri ninavyopata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…