Jamani napata tabu kutambua uelewa wa wabunge wetu! kwa kupitisha maamuzi kuwa kila mwaka ukienda kulipia vehicle licence ulipie pia gharama ya fire extinguisher takriban 40,000/= pasipo kupewa hicho chombo chenyewe si dhuluma kwa wananchi huku?
Mazingira nliyoyakuta TRA Kinondoni leo yamenisikitisha sana, kuona jinsi TZ nanavyoishi ktk zama za kale za mawe chini ya serikali hii ya CCM hadi karne hii ya sayansi na teknolojia!
Ndo kusema ingekuwa basi wanatoa hizo tanki basi kila mwaka wangetoa mpya?
Kwa dhuluma hii, naona SERIKALI ya CCM inateketea bado kuzimika tuu!
Wabunge wa CCM nchemba, lisinde and the like mnaopiga makofi ya ndioooooooo! kila hoja mpoooooooo!
TRA ni wababe na wanyang'anyi. Wakishaamua wameamua hasa kwa wananchi wa kawaida wa chini ambao uwezo wao ni mdogo. Hebu fikiria mwananchi kastaafu na imemchukua si chini ya miaka 2 kusubiri mafao yake na inabidi hata akope ili apate angalau nauli ya kufuatilia. Hatimaye anapokea mafao na anaamua kujinunulia Toyota Hiace ili imsaidie kufanya dala dala ili kujikimu kwa maisha yake yaliyobaki duniani.
Alipoagiza gari hiyo sheria ya wakati huo haikuwa na dumping fee yaani kodi ya uchakavu. Na kama ingekuwepo asingeagiza gari hiyo maana asingemudu gharama hivyo angeacha na kuangalia biashara ingine.
Sasa gari imeshaagizwa na imeshaingia mpakani kwa sheria ya zamani, mara TRA baada tu ya kusomwa general budget wanatangaza kuanza kwa sheria mpya kuanzia 1/7/2012 bila kujali kuwa tayari kuna wananchi tayari walishaagiza magari kwa sheria ya zamani na mengine tayari yalishafika nchini na utaratibu wa malipo ulishaanza kufanyika.
Ghafla unaambiwa ulipe tena 20% kodi ya uchakavu. Huyu mwananchi ambaye amepata pesa kwa kuokoteza atapata wapi pesa za ziada za kulipia?. Kama siyo ujambazi na unyang'anyi wa hata kidogo walichonacho wananchi ni nini?.
Kwa kuwa si rahisi kwa malipo hayo kufanyika kutokana na ukosefu wa pesa na hali ngumu ya maisha ina maana itabidi gari hiyo ibaki mikononi mwa TRA huku tayari lilishalipiwa malipo yote halali kwa sheria ya zamani. Na matokeo yake ni kupigwa mnada kwa gari hiyo na TRA.
Ni dhambi iliyoje kwa uonevu wa aina hii kufanywa na binadamu?. TRA wanapaswa kumwogopa Mungu la sivyo iko siku watalipwa kwa ubaya wao wa kinyama.
Kibinadamu. Kuanza kwa sheria mpya ya kuingiza magari ilipaswa kuwa specific si jumla jumla tu. Kama vile yale magari ambayo yangeagizwa na kuingia nchini baada ya tarehe 1/7/2012, yasingejumlishwa Pamoja na magari ambayo tayari yalishaingia nchini kabla ya tarehe hiyo tajwa.
Ni wananchi wengi wamekumbwa na kadhia hii. Na kama Serikali kupitia TRA ingekuwa sikivu kama inavyojinasibu mbele ya jamii wangeliangalia hili na kufanya marekebisho ili kuwapunguzia wananchi kadhia na mateso.
Nawasilisha.