Kwa wote wanaobeza vyuo binafsi, wanahitaji kurudishwa darasani...

Kwa wote wanaobeza vyuo binafsi, wanahitaji kurudishwa darasani...

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,126
kumekuwepo na wimbi kubwa la watu na hata mada zikibeza na kutilia shaka uwezo na ubora wa vyuo vya binafisi kiasi cha wengine kuviita majina ya ajabu ajabu.

kwa mkutadha huo nimeona bora niwaeleweshe wote wanaojigamba kwa majina ya vyuo vyao na si ubora wao kuwa elimu waliyoipata bado haijawasaidia na hawajakombolewa na kuwajengewa uwezo wa kufikiria,kung'amua na kutambua ukweli halisi ulivyo na nitawashauri warudi darasani wakasome upya ili wapate uwezo wa kuona mambo kwa usahihi wake.

BACK TO TOPIC.
napenda kuweka wazi ukweli huu na watu waniambie kama ni sahihi kwa wanavyofikiria.

1.mfumo wa elimu ya tanzania kuanzia form one mpaka form six unazipendelea shule za serikali kwa kuzipa nafasi ya kuchagua wanafunzi waliofaulu tu na makapi wanaachiwa ndugu zangu wa private.

-shule za serikali form one zinachukua wanafunzi walio na ufaulu wa juu na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaokosa kuchaguliwa kwa sababu ya marks zao kuwa za chini wanaenda kujaribu bahati yao private.

-matokeo ya form two necta yakitoka shule za private pamoja na kwamba ziliachiwa wanafunzi wengi wenye marks za kawaida zinaibuka kidedea dhidi ya shule za serikali ambazo zilichagua wanafunzi wazuri tu

-matokeo ya kidato cha nne yakitoka shule za private zinafanya vizuri tena kuliko za serikali pamoja na kwamba shule za serikali zilichagua wanafunzi wazuri tu.

MAELEZO HAYA YANATOA FUNDISHO KUWA ELIMU YA SERIKALI SI BORA KULIKO YA PRIVATE NA SERIKALI KAZI YAO NI KUHARIBU FUTURE ZA WATOTO ALAFU WANAWAACHA ILI TENA WAOKOLEWE NA PRIVATE SCHOOLS KIDATO CHA TANO NA SITA BAADA YA KUACHWA.

mimi mwenyewe ni mwathirika maana darasa zima tulikula za uso kwenda form one hakuna hata mmoja aliyepenya,ndipo wanafunzi watano tukaokolewa na private ya huko home na kati ya hao ni mmoja tu ndio alishia form four ila wengine walichanja mbuga mpaka vyuoni.

SABABU ZA UBOVU WA ELIMU SERIKALINI ZINAJULIKANA NA SITAZITAJA ILA ITOSHE TU KUSEMA KUWA SABABU NYINGI ZINAZOATHIRI ELIMU SEKONANDARI HATA KWENYE VYUO VIKUU VYA SERIKALI SABABU HIZO ZIPO NA ZINAFANYA KAZI YA KUPUNGUZA UFAULU WA WANAFUNZI HUKO ALAFU WENYE KUKOSA MAARIFA YA KUFIKIRI WANASEMA WAKIPATA GPA NDOGO NDO ELIMU ILIKUWA NZURI KUMBE WAMEATHIRIKA NA MAZINGIRA MABOVU ZIKIWEMO TARATIBU.

-wanafunzi wanaofeli form four kwa kupata angalau three ya mwisho na four za mwanzo serikali inawaacha ambao wengi wao ni wa shule za serikali na ndio hao serikali ilituambia ndio waliostahili kusoma ilipowachagua form one,hawa wanafunzi inabidi waende private kutafuta bahati yao huko, wengi wao kati ya hawa huwa wanafaulu tena na kuthibitisha kumbe wanaweza kufaulu ila walifeli kulingana na kusoma serikalini na si ajabu tena hawa serikali ikawataka.

KIFUPI NI KWAMBA PRIVATE SECTORS WAMEONYESHA UWEZO MZURI WA KUWAFUNDISHA WATOTO NA KUFAULU NA HAPA HAKUNA ANAEBISHA KWA SABABU WANAFUNZI WOTE WANASOMA KWA SYLLABUS MOJA NA MITIHANI NI ILE ILE ILA TATIZO LINAKUJA VYUONI AMBAPO WATU HAWANA SAME SYLLABUS NA MITIHANI YAO NI TOFAUTI NA NDIPO UNAANZA KUSIKIA MAJINA YA AJABU AJABU KWA HIVI VYUO KISA WANAFUNZI WAKE WANA GPA KUBWA.

mfano wanafunzi wanalundikwa lecture hall ukute wapo 400,humo wapo hawasikii kabisa najua maana wanafunzi wengi wanakimbilia mbele ili angalau wasikie na wakichelewa wanakaa nyuma na kusikia ndo inakuwa utata,wengine hawaelewi lakini hawawezi kusema hawaelewi na inabidi wakaushe tu nk nk alafu wakipata GPA ndogo wanalalamika wanapoona wale wa vyuo vya vitongoji wamepata GPA kubwa wakati wenzao walifundishwa darasani wanafunzi 40 tu,wasipoelewa wanauliza na wote wanasikia,lecturer akizingua ama haeleweki analipotiwa na kubadilishwa ama kutimulimuliwa.

mbona hamsemi mashule ya private yanavyofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa ambapo kuna mtihani mmoja?

ama huko hamuoni kama wanapata one na two wengi na hata one kali kali kiasi hata cha tanzania one wengi kutokea huko?

nini tofauti ya mifumo ya shule za private na vyuo vya private katika ufanisi?nini tofauti ya shule za serikali na vyuo vya serikali katika ufanisi?

mbona pia hamuulizi kwa nini shule za serikali pamoja na kujichagulia wanafunzi wazuri lakini bado zinafelisha badala ya kufaulisha?

ingekuwaje kama siku moja shule za private zichague wanafunzi waliofaulu alafu makapi yaende serikalini?watu wangetoka kweli?haki ya nani itakuwa kiama,naamini hata division four zinaweza kukosa kabisa kwenye necta na wanafunzi wote kubaki na zero.

ingekuwaje kama mfumo wa elimu ungetaka kuwa wanafunzi wa shule za binafisi waendelee kuwa wa binafisi mpaka vyuoni?kwa kuwa wanafunzi wa shule za serikali ndio wanaongoza kufeli je mpaka kufikia form six kuingia chuoni serikali ingebaki na asilimia ngapi ya wanafunzi ilioanza nao na je ingeonekanaje kama ubora ungeangaliwa kwa ufaulu tu kama wanavyofanya watu wetu wenye uwezo mdogo wa kufikiri?hizo one nyingi leo sizingekuwa private universities?

2.udahili wa vyuoni na hoja za wanaosema vyuo vya watu binafisi havina ubora.

-kwanza vyuo hivi vinadahili wanafunzi wenye marks za chini sana mpaka hata three za 17 lakini mwisho wanapata GPA kubwa za 4 na kuendelea(si maneno yangu bali ni hoja ya watu hao)

MAJIBU KWA HOJA HII.

kabla hujafikiri chochote kuhusu majibu kwa hili unapaswa kujua pia kwa nini shule za private zinachukua wanafunzi hata waliofeli la saba lakini wanaibuka na one?

unapaswa pia kujua kwa nini shule za private zinachukua wanafunzi wenye three za mwisho na div four kusoma advance alafu wanaibuka na division one na two na hata three kwa combination zote hata za sayansi?

HAPA SITAKI KUPIGIA DEBE SHULE NINAYOIJUA ILA NAJUA KAMA WATU NI WAJASIRI WATAKUJA HAPA KUTOA USHAHIDI KUWA WAO WALIPATA FOUR O LEVEL SHULE ZA SERIKALI ILA WAKAENDA PRIVATE NA KUIBUKA NA ONE AMA TWO YA FORM SIX NECTA NA WALIENDA UDSM AMA UDOM AMA MZUMBE AMA SUA.

UKISHAPATA MAJIBU HAYO NI VYEMA UKAJARIBU KUYAUNGANISHA TENA KWA MATOKEO YA GPA KUBWA ZA VYUO VYA BINAFISI.

JE UMEWAHI KUJIULIZA INGEKUWAJE KAMA VYUONI KUNGEKUWA NA PAPER MOJA KWA VYUO VYOTE?JE PRIVATE WANGEONEKANA MABOYA AMA WANAWEZA?hayo majibu kila mtu anayo yake.

-UBORA WA WANAFUNZI WA CHUONI UNAPATIKANA KWA VIGEZO VIPI HASA?

nimefatilia kwa kiasi kikubwa kwa wenye hoja hizi nikabaini wanaangalia matokeo ya wanafunzi ya kidato cha sita tu huku mengine wakiyaacha kabisa kuyaangalia.

NASEMA KUNA MAKOSA MAKUBWA SANA HAPA NA WATU HAWATAACHA KULALAMIKIA VYUO VYA BINAFISI KWA SABABU YA UFINYU WAO WA KUFIKIRI NA NDIO MAANA NIMESHAURI HAWA WARUDISHWE TENA SHULE UPYA WAKAJENGEWE UWEZO WA KUFIKIRIA.

MAPUNGUFU KATIKA HOJA YA MATOKEO KAMA KIPIMO CHA UBORA WA MWANAFUNZI.
-kwanza matokeo yanayotazamwa na wengi ni ya form six pekee,hawajui kuna wanafunzi wana one na two za form six na wapo udsm ama udom ama mzumbe ama sua ila form four walikuwa na four ama three za kuchechemea na waliokolewa na private, ama hawajui kuna wanafunzi wana three za 17 form six ila wana wana one za single digit O level ila kisa wapo vyu vya kitongoji ni tatizo.

SASA JE TUTUMIE MATOKEO YAPI KUSEMA HUYU MWANAFUNZI NI BORA?TUKITUMIA YA SIX NI MWAKE ATAONEKANA ALIFAULU VIZURI LAKINI TUKITUMIA YA O LEVEL NANI ATASEMA HUYU NI MWANAFUNZI BORA?
swali kwa nini mnatumia hasa matokeo ya kidato cha sita tu na mnasahau kuchukua historia ya matokeo yote mpaka ya form four?

mbona udsm ina watu walikuwa na four O Level ama nacho ni chuo cha kitongoji? NAJUA WATU WATASHANGAA HAPA LAKINI NDIO UKWELI WENYEWE.

KIDOGO NINGEPENDA KUELEZA KWA NINI UDSM INACHUKUA WANAFUNZI WENGI WENYE MATOKEO MAZURI YA FORM SIX.

kwanza udsm ni chaguo na ndoto za wanafunzi wengi kusoma hapo(ila haikuwa mimi) na sababu ni za kihistoria,mpaka leo ndicho chuo kinachojulikana na wengi hasa watu wa zamani ambao ni wazazi wetu kwa hiyo wengi tumejengwa tokea mwanzo kuwa hicho ndio chuo kikuu,ukisema kwingine wazee wanakushangaa sawa na watakavyomshangaa mtu atakaekuja hapa aseme yeye ni engineer wa kemikali mana wao wanajua injia ni yule wa civili engineering tu.

kwa hiyo udsm inapata request nyingi sana na wote tunajua utaratibu wa kuchagua ni kuanza na aliye bora zaidi kushuka chini,japo nao udsm wanaangalia sana matokeo ya six na ndio mana hawajali sana kama o level uligonga four ama three ya mwisho.

na sababu nyingine ni kwamba udsm ina uwezo mdogo wa kuchukua wanafunzi wanaostahili kusoma degree,na ninawahakikishia kuwa hata wanafunzi wenye div three za 17 wapo eligible kusoma udsm kama tu wana C tatu O level na principle mbili Advance ila kutokana na uwezo mdogo wa udsm ku accomodate wanafunzi ndio inawaacha.

-sababu zilizopelekea hawa wanafunzi waliofeli kufeli hazizingatiwi katika kuangalia ubora wa wanafunzi,mtu katoka shule ya serikali haina hata walimu amekomaa mwenyewe akapata three yake ya 17 alafu unasema hana uwezo wa kupata GPA ya 4.5 kumbe anao uwezo kama akifundishwa na kupewa kila kinachostahili. na wanapofika vyuo vya private elimu inaonekana kumbe ni nyepesi maana wanafundishwa vizuri,sasa kwa ni nini wasifaulu na kupata GPA ya 4?

ngoja nitoe mfano mmoja,kuna shule moja kali ya private arusha nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni sister(katoliki) na yeye ndo alikuwa mkuu wa shule ile,ilikuwa kipindi cha kuchagua wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza.
kwa kuwa ananiamini sana akaniambia nisahishe mitihani ya kiingereza nikakataa,baadae akaniambia nisahishe ya hesabu nikakataa ila akanilazimisha,ikabidi nikubali,nikasahisha na marks za wanafunzi wote zikawa tayari.

sasa vigezo vya shule ile kuchagua wanafunzi ndio vilinishangaza ila nikajifunza kitu baada ya kuelekezwa.

-kwanza wanaangalia mwanafunzi katoka wapi?na shule ipi?na kukoje huko?hapa wanaweza kumchukua mwanafunzi hata mwenye marks ndogo kabisa ila ameonyesha uwezo fulani baada ya kuangalia alikotoka na kubaini kuwa huyu katoka eneo ambalo elimu iko chini sana na hivyo atakuwa mzuri ila mazingira ndio yanamfanya asijue. ama wanaweza kumuacha mwanafunzi mwenye ufaulu wa wastani aliyetoka shule bora kabisa japo amefikisha marks kwa kuangalia kuwa amepata marks za kawaida sana pamoja na kuwa katika mazingira bora zaidi na shule bora zaidi.

sister akanipa mfano wa mwanafunzi aliyekuwa form three wakati ule 2012 ambaye ndio alikuwa akiongoza darasani,akaniambia yule mwanafunzi alipata marks ndogo sana ila walilazimika kumchukua kwa kuwa waliona katokea ndani kabisa maporini huko arusha kwa wamasai ambako elimu ni kitendawili na walihisi atakuwa mzuri sema tu huko elimu ni mbovu kupindukia,alipoanza form one wakadili nae kumfundisha english kwa ukaribu zaidi na baada ya mwezi wa sita tu akaanza kuongoza mitihani ya shuleni licha ya mwanzo kuanza na namba za mwishomwisho,aliongoza necta ya form two na hata form three bado alikuwa moto.

NADHANI PIA MMEJIFUNZA KITU HAPA JUU YA UBORA WA MWANAFUNZI KUWA UNATEGEMEA MAMBO MENGI SANA NA HATA UFAULU WA MWANAFUNZI UNATEGEMEA MAMBO MENGI SANA IKIWEMO YEYE MWENYEWE NA MAZINGIRA YA SHULE AMA CHUO

MWISHO NINGESHAURI WATU MJIPAMBANUE KWA MAFANIKIO YENU BAADA YA KUMALIZA VYUO KAMA UBORA WA ELUMU YENU NA SI KULAZIMISHA KUPATA SIFA KISA UMESOMA CHUO FULANI AMA KUMUBEZA MWINGINE KISA KASOMA CHUO FULANI.

tunataka akina Stive Jobs hapa,tunataka kina Newton hapa,tunataka kina Eisten hapa,tunataka kina GALILEO GALILEI hapa na wengine wengi,hatutaki majina ya vyuo ama shule. show your quality of education to innovations and is when we shall appriate your quality.

udsm ni 4 africa,is the best university.

in which category?baanisha ili nijue cha kuchangia ama weka link,maana watu huwa hamjui hata vigezo vinavyotumika na wakati mwingine vigezo vya ranking ni mambo ya ajabu ajabu,kama kuna jamaa aliweka ranking ya vyuo vya africa alafu nilipofungua link nikakuta kigezo kilikuwa umaarufu wa vyuo na walifanya utafiti wakakiri kuwa vyuo vilivyotawala kwenye namba za mwanzo si vyuo bora japo wengi waliiona ni maarufu na humu udsm imo ,sasa hapo ndo nini,pia kuna vigezo vingine huwa wanatumia ku rank ubora wa vyuo kama idadi ya research zinalizofanywa na wahitimu wa vyuo husika,

sasa hapo huoni kama vyuo vya tangu zamani lazima viwe na watu wengi kwa kuwa vina wahitimu wengi waliowahi kufanya tafiti kuliko hivi vyuo vya private ambavyo vimeanzishwa muda si mrefu lakini vimejitahidi sana kuweka miundombinu bora na vifaa bora na walimu wakutosha.

alafu mbona unachangia kitoto sana?ina maana pamoja na kusoma udms na sijui ni undergraduate ama una degree ama una masters nk bado huwezi kuchangia kwa kujenga hoja?ama ndio ubora wa wanafunzi wa udsm?unakiabisha chuo na wanafunzi wengine wa hapo
 
nimekuelewa ndugu,,,,ukweli ni kwamba najutaa kuja UDSM hamna kitu cha maana hapa darasani tunarundikwa kama nini......bora hata st joseph nasikia 35 tu darasani,,,,mwanangu lazima aende pale
 
.......chuo ni chuo haijalishi kama private au public, as long as mnatumia materials
yale yale kwenye masomo. Vitabu ni vile vile nini kinachoweka utofauti?
 
asilimia kubwa ya wasomi wa nchi hii hawajui nini maana ya elimu,elimu ni kile kitu kinacho baki kichwani baada ya kumaliza masomo yako,wao wanabaki mimi nimesoma chuo bora bhan,utasikia aah nimesoma UDSM AU MZUMBE, onyesha huo UDSM wako kwenye kuto material uliyo nayo kichwani wewe wa UDSM uliesoma labda BBA,PR,TOURISM, uwekwe pa1 na mwanafunzi aliesoma SAUT,TUMAINI,ST JOHN au RUCO aliesomea kozi hizo hizo ulizossomea wewe arafu kila mmoja awe anaonyesha kile alichokisoma,co kelele tu arafu asilimia kubwa vichwani hamna kitu,pia ni vizuri mjue nini maana ya neno university pia lilianzia wapi na lina maana gani
 
mpiga msuli kuja huku upate majibu ya hoja yako kuwa kwa nini private wanapata matokeo mazuri
 
asilimia kubwa ya wasomi wa nchi hii hawajui nini maana ya elimu,elimu ni kile kitu kinacho baki kichwani baada ya kumaliza masomo yako,wao wanabaki mimi nimesoma chuo bora bhan,utasikia aah nimesoma UDSM AU MZUMBE, onyesha huo UDSM wako kwenye kuto material uliyo nayo kichwani wewe wa UDSM uliesoma labda BBA,PR,TOURISM, uwekwe pa1 na mwanafunzi aliesoma SAUT,TUMAINI,ST JOHN au RUCO aliesomea kozi hizo hizo ulizossomea wewe arafu kila mmoja awe anaonyesha kile alichokisoma,co kelele tu arafu asilimia kubwa vichwani hamna kitu,pia ni vizuri mjue nini maana ya neno university pia lilianzia wapi na lina maana gani
Good good comment hapo umenena wasomi tuna bla blah sana
 
nimekuelewa ndugu,,,,ukweli ni kwamba najutaa kuja UDSM hamna kitu cha maana hapa darasani tunarundikwa kama nini......bora hata st joseph nasikia 35 tu darasani,,,,mwanangu lazima aende pale
ukweli ni kwamba ili ujue raha ya ngoma ingia ucheze.sie tulio huku tunapatamani lakini kadri siku zinavyoenda sijutii umuhimu wangu kuletwa St.joseph maake watu 400 hall moja si kazi rahisi.Sizani hata kama ma lecturer wanazingatia usahihishaji wa mitihani yao sababu number hiyo ni kubwa mno
 
Hoja yako ina mashiko mimi ni moja wa waangwa wa matokeo ya O Level nilikuwa shule ya govt nilibahatika kuendelea na A Level na nikapata matokeo mazuri hata watu hawakutegemea ila mi nilijua changamoto zilizokuwa zina nikabili ni kweli anaye beza private institutions hayupo sawa coz wanafanya vizuri sio katika Elimu tu bali Afya, Viwanda na nyinginezo.Naunga mkono hoja yako mkuu
 
Ujinga mtupu vyuo vya private vimekuja kuharibu elimu TANZANIA maana mpaka wenye iv.18 nao wanaingia chuokikuu na pia takausitake vyuo vya PRIVATE wanagawa miG.P.A kwa sababu vipo kibiashara zaidi
 
.......chuo ni chuo haijalishi kama private au public, as long as mnatumia materials
yale yale kwenye masomo. Vitabu ni vile vile nini kinachoweka utofauti?

Wewe hapanaaa vyuo vya private havina maana vimekuja kuharibu elimu tanzania, unakuta WAHADHIRI wanawapa miG.P.A mikubwa kuliko uwezo
 
Ujinga mtupu vyuo vya private vimekuja kuharibu elimu TANZANIA maana mpaka wenye iv.18 nao wanaingia chuokikuu na pia takausitake vyuo vya PRIVATE wanagawa miG.P.A kwa sababu vipo kibiashara zaidi

kumbe upo kuandika matusi,nipo hapa kujadili hoja,matusi ni option ya aliyeshindwa kujenga hoja,ebu kaangalie top ten darasa la saba kama utakuta shule hata moja ya serikali?zinaanzia kwenye 1000 na kitu,ebu kaangalie matokeo ya form two uone aibu ya institution za serikali,ebu kaangalie shule matokeo ya form four shule iliyofanya vizuri ya serikali imeanzia 40,kwa kuwa huku kuna paper moja hakuna hata mjinga mmoja anaekohoa wala kuuliza kama wanafunzi waliofaulu vizuri shule za private walikuwa matokeo mabovu nyuma
 
Wewe hapanaaa vyuo vya private havina maana vimekuja kuharibu elimu tanzania, unakuta WAHADHIRI wanawapa miG.P.A mikubwa kuliko uwezo

unataka wapewe failure ama GPA ndogo hata kama wamefaulu?unajuaje kuwa wana uwezo usiolingana na GPA zao?
 
kumbe upo kuandika matusi,nipo hapa kujadili hoja,matusi ni option ya aliyeshindwa kujenga hoja,ebu kaangalie top ten darasa la saba kama utakuta shule hata moja ya serikali?zinaanzia kwenye 1000 na kitu,ebu kaangalie matokeo ya form two uone aibu ya institution za serikali,ebu kaangalie shule matokeo ya form four shule iliyofanya vizuri ya serikali imeanzia 40,kwa kuwa huku kuna paper moja hakuna hata mjinga mmoja anaekohoa wala kuuliza kama wanafunzi waliofaulu vizuri shule za private walikuwa matokeo mabovu nyuma

Kweli wewe umesomea vyuo vya private ndio maana mvivu wa kufikiri! Mfumo wa sekondari ni tofauti na chuokikuu ,sekondari na msingi wanakuwa chini ya mfumo mmoja ambao ni NECTA! wakati CHUO KIKUU mitihani na usahihishaji unasimamiwa na chuo husika kwa hiyo inakuwa rahisi kuwapa marks kubwa wanafunzi
 
wewe huoni kama kuna tatizo katika institution zote za serikali?ni nchi gani duniani ambapo vyuo ama shule za serikali zinashinda ubora wa institution za serikali?kungekuwa na paper moja alafu private university wakifanya izuri kuliko serikali ungesemaje?najua kuna tofauti kwenye ngazi tofauti za elimu ila najua hujasoma maelezo yote mana kila kitu nimejibu, hata kwenye mashule ya serikali watoto wanapata marks ndogo kwenye mitihani ya ndani wakati wa private wanapata marks kubwa kwenye mitihani ya ndani na matokeo haya yanabaki hivi hivi hata wakifanya NECTA,kama private waliweza kuzifanya shule zao zipate matokeo mazuri kwa nini washindwe kuvifanya vyuo vyao vipate matokeo mazuri?
 
Ngoja nikwambie nasema laiti kungekuwa na mtihani wa pamoja let say ACCOUNTING,ENGINEERING,LAW, n.k hakuna hata chuo kimoja cha private kingeweza kufanya vizuri zaidi ya vyuo vya private hawa watu ni vilaza sugu ! wanashindwa hata maswali madogomadogo! chuo kinachukua watu wenye one za 3,4,5
 
in law we have law school exams,HAO SAUT hawafaulu?in engineering we have ENGINEER REGISTERING BOARD EXAM,hao st.joseph hawafaulu?bisha kwa hoja,kwani uwezo wa mtu unapimwa kwa matokeo ya six tu?udsm kuna watu wana 4 za o level,private kuna wengine wana one single za olevel,lazima ujue kwa nini walifaulu ama walifeli katika mazingira gani.
 
Back
Top Bottom