GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Je;
1. Simba SC icheze mpira wake wa Samba Loketo ila ifungwe au iambulie sare/suluhu kisha timu na mashabiki tuvurugane zaidi, tuchapane bakora, tuchekwe na watani zetu Yanga SC na mgogoro uzidi Kukua.
au
2. Simba SC icheze vibaya kama ilivyocheza leo (tena ikiwa ugenini) Jijini Kampala dhidi ya timu ambayo ilikuwa inahitaji ushindi wa udi na uvumba na ipate Ushindi wa goli/bao moja iliyoupata ili kutuliza hali mbaya kikosini, kwa uongozi na kwetu mashabiki akina GENTAMYCINE, kisha kurejesha morali kwa wapiganaji wetu (wachezaji) na kurejesha saikolojia iliyopotea ghafla kwa wachezaji.
Ili tukirejea Dar es Salaam tutulie, tumalize tofauti zetu, tushirikiane na tuunganishe nguvu zetu, ili alama sita (6) muhimu za Vipers FC na Horoya FC kwa Mkapa tuzipate na tuwe na jumla ya alama tisa (9) ambazo zitatupeleka Knockout Stage (Robo Fainali) ya CAFCL kisha tuendelee kulinda heshima yetu, kuitangaza vyema nchi yetu na kuongeza alama (points) zaidi ambazo zitasaidia Tanzania kama nchi kuingiza tena timu nne (4) kwa msimu ujao wa mashindano.
Nasubiria majibu yenu ila niseme tu kuwa kwa hali iliyokuweko Simba SC kabla ya Mechi yake dhidi ya Vipers FC leo nilitegemea wana Simba SC wote tungeanza kuhamasishana ili twende kuwapokea mashujaa na wapiganaji wetu (Wachezaji wa Simba SC) kwa huu ushindi muhimu wa leo dhidi ya Vipers FC tuliokuwa tunauhitaji kwa kumuomba Mwenyezi Mungu na mizimu yetu ya Kizanaki, Kimakuwa na Kitutsi.
Wachezaji wametuheshimisha mno.