Kwa yeyote mwenye uzoefu wa biashara ya kuku wa kienyeji anijuze!

Fure

Member
Joined
Apr 1, 2013
Posts
23
Reaction score
7
Habari zenu wa ndugu?
Kwa yeyote mwenye kujua biashara ya kuku wa kienyeji kwa yule anaye nunua na kwenda kuuza sehemu nyingine.

Mwaswali yangu ni je,
1. Kuku wa kienyeji wanapatikana wapi kwa wingi katika nchi yetu (tz)?

2. Manunuzi yao yakoje(bei yao ya jumla ni shl ngapi na wanakuwa wa ngapi au mmoja ni shl ngapi?

3. Ghalama za usafiri kutoka huko walipo mpaka dar ni kiasi gani kwa makadilio ya kawaida?

4. Mwisho naomba kujua mtaji wa chini kabisa kuanzia hiyo biashara ni shl ngapi? (nikimaanisha mm mwenyewe nitoke dar niende huko na kisha nirudi na huo mzigo)

naomba kujua wadau nasubiri majibu yenu asanteni!

Kauri mbiu ya mwaka huu, 'hapa ni kazi tu' nataka nianze hiyo kazi mara moja!
 
Jamani wanao jua waje watujuze ni wengi tunao taka kujua hizo gharama!
 
Kuku wa kienyeji 6000, mpaka elf 9000 wakifika dar bei ni kuanzia 9000 mpaka 1400 kumbuka bei ya mtetea ni tofauti na jogoo pia ukubwa wa kuku na uzito unachangia bei kuwa kubwa

=> kuku ni singida

=> usafiri mzuri ni malori ya usiku kumbuka biashara yoyote mzigo ukiwa mkubwa ndo utapata faida yake vizuri
kwahiyo ukichukua kuku wachache faida ndogo na utakata tamaa

=> kumbuka kuku wanauzwa vijijini wanahitaji watu wa kuwakusanya ni bora ukatafuta mawakala wa singida akusafirishie upokelee dsm, japo kuna matapeli ktk biashara
 
ni bora ukatafuta mawakala wa singida akusafirishie upokelee dsm, japo kuna matapeli ktk biashara

Nashukuru sana kwa kunijuza, sasa jinsi ya kuwapata hao mawakala wahaminifu apo ndio shidaaaa..... cjui nitumie njia gani ili niwapate
 
duuh biashara nzuri hii mawakala kuwapata ni huko huko mara ya kwanza pili lazima uende mwenyewe kwanza
 
Mie mzoefu sana kwenye hii biashara ila kwa sasa nakula mafao kwanza.
Kuku wengi ni singida na Tabora,
Singida kuna vijiji vina breed nzuri ila pia kuna sehemu mbegu ni kuku wadogo sana.

Katika biashara yangu sijawahi kukutana na bei ya jumla,ila bei ya kujumua katika minada,bei inategemea na msimu, kuna kuanzia 5000-10000

Gharama itategemea na usafiri unaotumia,either magari ya mizigo yanayopita yakiwa matupu kuelekea Dar,ama bus ambako hauwezi kusafirisha mzigo mkubwa na wana gharama kubwa.

Mtaji itategemea kama mzigo utaufuata mwenyewe ama utakua na agent au ulivyopanga wewe.
Karibu.
 
asante kwa kunijuza na hongera kwa kula mafao!
je, changamoto zake ni zipi? Na je kunahitaji leseni ya biashara wakati unafuata huo mzigo?
 
Ahsante,
Leseni sijawahi kuwa nayo wala kuulizwa,
Ila huwa kuna ushuru wa mnadani.
 
asante, sasa huo ushuru wa mnadani ni kwaajiri ya mtu anaye nunua au yule anaye uza? ok na huwa wanalipa kama shl ngapi?
 
Ni anayenunua,kuku mmoja 500 ila Mara nyingi unawakazia unawapa 2000 unaondoka
 
Mie mzoefu sana kwenye hii biashara ila kwa sasa nakula mafao kwanza.
Kuku wengi ni singida na Tabora,
Singida kuna vijiji vina breed nzuri ila pia kuna sehemu mbegu ni kuku wadogo sana.

Katika biashara yangu sijawahi kukutana na bei ya jumla,ila bei ya kujumua katika minada,bei inategemea na msimu, kuna kuanzia 5000-10000

Gharama itategemea na usafiri unaotumia,either magari ya mizigo yanayopita yakiwa matupu kuelekea Dar,ama bus ambako hauwezi kusafirisha mzigo mkubwa na wana gharama kubwa.

Mtaji itategemea kama mzigo utaufuata mwenyewe ama utakua na agent au ulivyopanga wewe.
Karibu.
Mfano kusafirisha kuku 30 toka singida mpk morogoro town ni shilingi ngapi ktk lorry?
 
Kwenye Lori ni makubaliano
Nilikua na jamaa zangu

Kwenye basi mmoja ni 1000
 
Okey km inawezekana nipatie namb za mmoja anayesafirisha kwa lorry pia km utakua na namb ya mfugaji yyt singida.
My no 0717 012 885
 
Mie mzoefu sana kwenye hii biashara ila kwa sasa nakula mafao kwanza.
Kuku wengi ni singida na Tabora,
Singida kuna vijiji vina breed nzuri ila pia kuna sehemu mbegu ni kuku wadogo sana.

Katika biashara yangu sijawahi kukutana na bei ya jumla,ila bei ya kujumua katika minada,bei inategemea na msimu, kuna kuanzia 5000-10000

Gharama itategemea na usafiri unaotumia,either magari ya mizigo yanayopita yakiwa matupu kuelekea Dar,ama bus ambako hauwezi kusafirisha mzigo mkubwa na wana gharama kubwa.

Mtaji itategemea kama mzigo utaufuata mwenyewe ama utakua na agent au ulivyopanga wewe.
Karibu.
Kaka naomba uzoefu wako ,wilaya ya kisarawe ndanindani kuku wanapatkana kwa bei hyo ya elf 6 mpaka 9 mimi naomba unisaidie ishauri kama ifuatavyo
1. Usafi mzur kuwaleta dar
2. Taratibu za kusafirisha ( vibali, leseni n.k )
 
Kwa kisarawe sifahamu kabisa

Ninachojua kama unawachukua mnadani utawalipia ushuru
 
Kwa kisarawe sifahamu kabisaundefinedNinachojua kama unawachukua mnadani utawalipia ushuru
undefinedunatumia cage hizi za kienyeji au una zile cage za plastic kusafirishia kuku?
 
Back
Top Bottom