Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Maalimu ni mjanja sana. Aligundua uchu wa CHADEMA wa kupata urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kupitia mgombea wao Tundu Lissu.
Deal likapigwa kati ya Maalimu na Mwamba la 'ushirikiano' kufikia adhima hiyo. Makubaliano (MOU) yakafikiwa kwamba:
1. CHADEMA imuondoe mgombea wao wa kiti cha urais wa Zanzibar na wafuasi wao (CHADEMA) walioko Zanzibar kura zao wampe Maalim. Hili litamwongezea chance ya Maalimu kushinda urais huko Zanzibar.
2. In reciprocate to CHADEMA, wafuasi wa ACT Wazalendo walioko Tanzania bara kura zao watampa mgombea urais wa JMT kupitia chama cha CHADEMA na bila shaka wabunge na madiwani wa Chadema. Akawaaminisha Chadema kuwa kwa kufanya hivyo Chadema itakiondoa chama cha CCM kutawala huko bara.
CHADEMA wakajifanya kama vile hawajui kwamba:
1. Urais wa Zanzibar na urais wa JMT ni vitu viwili tofauti sana. Rais wa Zanzibar anachaguliwa na wakazi wa Zanzibar peke yao na mamlaka yake ni kwa mambo ya Zanzibar yasiyokuwemo kwenye mambo ya muungano yaliyoainishwa kwenye katiba ya JMT.
2. Rais wa JMT anachaguliwa na wananchi wote wa Tamzania visiwani (Zanzibar) na Tanzania bara - walio kwenye vyama mbali mbali vya kisiasa na wale ambao hawako kwenye chama cho chote cha kisiasa. Hivyo hata kama wafuasi wote wa ACT wazalendo walioko huku bara wakampa Lissu kura zao hakutakuwa madhara ye yote kwani wafuasi hawa ni wachache sana, negligible.
3. Makubaliano hayo yatakifuta kabisa ACT-Wazalendo huku Tanzania bara kwani yanamaanisha hakutakuwanna mgombea urais, ubunge na udiwani kupitia chama hiki ambaye atapata kura za wafuasi wa chama chake; watawapa kura zao wagombea wa chadema.
4. Hivyo ACT Wazalendo huku bara itakuwa imefutika na kubaki jina tu. Itakuwa imeshachukuliwa na akina Maalimu huko Pemba. Huyu Maalimu ni mjanja sana. Alimfanyia hivyo muazilishi wa chama cha wananchi (cuf) Bw. Mapalala miaka ile. Lipumba akaja kuirudisha ikiwa hoi. Sasa Zitto naye ndivyo hivyo kaisha nyang'anywa chama chake alichokianzisha na akina Maalimu wakishirikiana na Mwamba wa chadema aliyemtimua huko chadema enzi zile.
Hili ni deal safi kutokea msimu huu.
CC: Membe & Zitto