Uchaguzi 2020 Kwaheri Charles Mwijage, Ubunge sio cheo cha Ufalme

Uchaguzi 2020 Kwaheri Charles Mwijage, Ubunge sio cheo cha Ufalme

Mchumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
280
Reaction score
262
Serikali ya awamu ya tano chini ya Dr John Magufuli wakati ikipambana kuhakikisha nchi inakua kiuchumi kuna baadhi ya viongozi wa ovyo wao akili zao wanawazia nafasi za uongozi wao. Ni tarehe mbili mwezi wa saba tu mwaka huu Tanzania inafanikiwa kuingia kwenye uchumi wa kati wa chini ambapo tangu Tanzania ipate uhuru tulikuwa hatujawahi kufikia hatua hiyo.

Wakati Mwijage anatumbuliwa kwenye cheo cha uwaziri baadhi ya watu walijua alionewa lakini kwenye jimbo la Muleba Kaskazini siku hiyo ilikuwa ni ya nderemo na vificho kwa wananchi kutokana na kutumbuliwa kwake. Charles Mwijage ni wabunge ambao ni dhaifu lakini alibahatika kuaminiwa na serikali na kupewa majukumu makubwa ambayo hayaendani na uwezo wake. Ni waziri ambaye alishindwa kupafomu vizuri wilayani kwake wakati akinadi kampeni ya Tanzania ya viwanda nchini huku yeye mwenyewe anaua viwanda vinavyojengwa wilayani kwake kwa kuogopa kwamba watachukua nafasi ya ubunge.

Mwijage akili yako imechoka na uwezo wako umeishia hapo, achia nafasi kwa watu wengine wenye nguvu na maono. Ni aibu kuwa na mtu ambaye kamuangusha Rais wetu katika utendaji kazi. Umeshindwa kwendana na kasi yake waachie watakaoweza wafanye hiyo kazi. Sasa hivi umeishiwa hoja unakimbilia siasa za matusi, fitina na kuendekeza chuki kwa wananchi. Siasa za hivyo zimepitwa na wakati ndio maana kwa sasa unatumia nguvu nyingi kumwaga pesa ili watu wakupende. Uongo na ukweli havikai pamoja. Mwijage wewe ni muongo na huo uongo wako umekua ukijisifia kuwa ni propagandist.

Sasa hivi unalia na kulalamika kwamba watu wanataka hicho kiti cha ubunge, Miaka 10 uliyofanya yanatosha kuendelea kutaka hicho kiti ni kudhihirisha usemi wako uliozoea kusema kuwa lazima watakupa kura tena kutokana na ujinga wao. Watanzania siyo wajinga na hii nchi ni ya demokrasia lazima utoke waingie wengine hiki siyo kiti cha ufalme. Je kama Rais alikuamini na ukamuangusha je sasa hivi ndio kusema umepata mbadala wa matatizo yote.

Miaka 10 ni mingi sana kwako utakumbukwa kwa propaganda chafu ambazo zinarudisha nyuma maendeleo. Tumeingia kwenye uchumi wa kati hatutaki kurudi nyuma kama ilivyo kwenye dira ya taifa tunahitaji viongozi wabunifu na wenye fikra chanya kwa maendeleo ya watanzania.

Muleba `kaskazini ni kubwa kuliko Mwijage kuwa mpole tumia pension yako vizuri katika kustaafu kwako. Umewaumiza watu wengi kwa roho mbaya yako na watu wanaokuzunguka kwa kuangalia maslahi yako. Tunajua hauna uchungu na Muleba Kaskazini bali unataka kuendelea kujinufaisha kutokana na uchu wako wa madaraka. Watia nia ni wengi mwaka huu. Kwa taarifa yako hutaweza kupita kwa visiki vilivyopo Muleba `kaskazini.

Kama siku ya kuvunja bunge ulisahau kupiga picha pole sana. Imeishakula kwako mzee.
 
Acha kutumika vibaya na watia nia, Mwijage bado anastahili kutuwakilisha wana Muleba Kaskazini, wewe haupigi kura jimboni. Wajumbe wa kupiga kura za maoni watampitisha tu Mheshimiwa Mwijage, wewe ulie tu
 
Tafta kavideo ka wazee juzi walimwashia moto kapo YOUTUBE KAWEKE hapa walitaka kumchapa
 
Ktk wabunge ambao niliona wana porojo nyingi mdomoni ila vitendo ni chini ya ziro basi mwijage mmoja wapo..
 
98% ya Wahaya ni watu wanyenyekevu na wastaarabu sana. nawajua kwa vile familia yangu imeoa na kuolewa katika jamii hiyo.

lakini kuna hii 2% ambao traits zao zinaonekana zaidi na unfortunately zinatishia hata kuwafunika hao 98%.

sad.

Mwijage yumo kwenye hiyo 2%!
 
Huyo jamaa nisha wahi muona masaki kalibu na hospital ya macho.
sasa kwa maisha alo nayo hata asipo kua mbunge hawezi kufa na njaa
 
Dah, huu usemi wake "lazima watampa kura tena kutokana na ujinga wao". umenisikitisha sana, Ina maana ka2aona wapiga kura wake mazuzu au??
 
Dah, huu usemi wake "lazima watampa kura tena kutokana na ujinga wao". umenisikitisha sana, Ina maana ka2aona wapiga kura wake mazuzu au??
 
Mafundi bomba mtauana,kachukueni fomu kwanza mpite kwenye kura za maoni
 
Charles Mwijage amejaribu na sasa inatosha. Ubunge sio ufalme. Amwachie mwana Muleba Kaskazini mwingine atuwakilishe.
Acha kutumika vibaya na watia nia, Mwijage bado anastahili kutuwakilisha wana Muleba Kaskazini, wewe haupigi kura jimboni. Wajumbe wa kupiga kura za maoni watampitisha tu Mheshimiwa Mwijage, wewe ulie tu
 
Back
Top Bottom