Kwaheri Irene, nyuma yako mbele yetu, Innalillah Wainna Illah Rajuun, tusipuzie wanaotaka msaada na kuita matapeli

Alexido jz instagram

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2026
Posts
4,686
Reaction score
10,018
Humu jf Kuna watu wana roho ngumu na mbaya sija pata kuona eti hadi I'd za kike, dah.

Kipindi Fulani nilitukanana na jamaa humu, Kuna mtu alitaka msaada, jamaa akaanza kumita tapeli nikamvaa nikamwambia bro kama una wasiwasi usitoe sio uwe chanzo cha wengine kutotoa.

Mapema majuzi nilikua naperuzi, insta, nika kutana na picha ya huyu dada, inasemekana anaitwa Irene, alikua mgonjwa, kazidiwa nyumbani kwake alipo kua amepanga majirani wakajichanga, wakampeleka hospitali, ndugu zake wakaanza kutafutwa kupitia mitandao kama Kuna mtu anamjua afike hospitali, Kwa bahati nzuri juhudi ikafanyika insta na fb Huwa haziniangushi asee salute mark, boss kubwa, kutoka united statesπŸ‡ΊπŸ‡², ndugu wakapatikana, mama mzazi akawasili dar, masikini Kwa bahati mbaya, Irene kafariki, namshukuru MUNGU Irene atazikwa na ndugu zake INSHAALLAH na si ile ya kutupiwa kwenye mashimo na kirundikwa na manispa, mwenyezi MUNGU tusimamie wapambanaji tulioko mbali na nyumbani kwetu, tujitahidi kuwa tunawasiliana na ndugu na kumuomba MUNGU inshaallah.

Punguzeni midomo na ujuaji, shukrani majirani Kwa kusimama show bila kujali dini kabila au chama cha siasa, MUNGU awabariki watanzania wote mliofanikisha hili.

Nawatakia sikuku njema ya idd njema inshallah

 
R.I.P IRENE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…