Kwaheri Simba SC, Ahsante kwa kushiriki michuano ya Mabingwa, CAF

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kwa kikosi dhaifu kilichojaribu kujitutumua mbele raja Casablanca kilipigwa nje ndani kwa jumla ya magoli sita kwa moja. Kila nikimtazama beki onyango na inonga naona kabisa ni ukuta mbovu ulioezekwa kwa mabua ni ngumu sana kuizuia wydad endapo itapangwa nayo.

Mchezaji Chama aliyemlazimisha Kocha aingie kwenye mfumo wake,
Ndiyo mchezaji huyo huyo anaezurura kwenye mechi za kibabe, ambazo zinabest players kuliko Mtibwa Sugar. Naona kabisa huyu hana uwezo wowote endapo atakutana na beki za Mamelodi.

Kila nikimtazama Sadio Kanoute, Mzamiru na Kibu Denisi nazidi kuishiwa nguvu kabisa naona ipo kazi kubwa sana endapo watakutana kikosi Cha waarabu waliofuturu vizuri, hakika naona aibu Mimi.

Huku Mo Dewji akiwananga Wana simba nakusahau kabisa kuwa alitoa pesa kichele katika usajiri nakusajiri akina kibu, Sawadogo nk. Leo hii kwa michuano mikubwa ya ligi ya mabigwa unadhani utafika nusu?

Hakika Sina Cha kusema ila nawapa mkono wa kwaheri mkajipange tena watani. Msikubali kuletewa manzoki na ahadi za kuifunga yanga badala ya kusajiri wachezaji kwa ajiri ya kimataifa.

Mtani huwezi kufika nusu kwa kuingia kinyumenyume ndani ya uwanja, kuchoma uwanja. Nasema tena kwa heri Simba SC ahsante kwa kushiriki michuano ya kimataifa.
 
Ijapo mimi sishabikii wa hizi team zenu mbili na league yenu kiujumla lkn nimegundua kuwa WEWE SIYO SHAABIKI WA MPIRA. WEWE NI MPAMBE WA WA TEAM.

KWA NINI UNAJITESA WAKATI HUNUFAIKI?
Hizo team Al Aily na Simba zitakutanaje?
 
Hivi hamchoki tuu? Maana hilo neno timu zaifu haifiki popote nimeanza kuwasikia tangu tunaenda kucheza na nyasa bulets chini ya kocha nguli mgunda. Simba akili kubwa, wakati nyie mnaiwinda kwenye hesabu za MAGAZIJUTO wao wenyewe simba wanawakwepa kwenye hesabu za BODMAS
 
Hivi hamchoki tuu? Maana hilo neno timu zaifu haifiki popote nimeanza kuwasikia tangu tunaenda kucheza malawi na nyasa bulets chini ya kocha nguli mgunda. Nyie uto hamuwezi ielewa simba kwani akili yenu ni ndogo huku simba ikiwa na akili kubwa
Nyasa bullets nayo timu yakujivunia ushindi [emoji41]
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1680577235752.jpg
    100.4 KB · Views: 6
Acha mambo ya kiwaki hayo. Tangu ume left group umekua na mambo ya ajabu na kiduanzi sana.
 
Dah mbona unatumia nguvu kubwa sana kubadili uongo kuwa kweli.
 
Al ahaly na Simba wakutane wapi? Kuna watu hawafuatilii hata michezo
Aliyesema wanakutana nan hapo nimezungumzia kwa ujumla kulingana na kikiosi Cha simba na wachezaji wa timu kubwa, elewa kolo wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…