Kwaheri Wayne Rooney japo usitegemee kuenziwa Manchester United

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,274
Reaction score
6,595
Kwaheri ya kuonana Wayne Rooney,ulijitoa kwa nguvu na maarifa makubwa sana kwa kipindi chote ulichoitumikia Man United(2004-2017) ..


Ulijitahidi kuziba pengo la Ronaldo na kwa kiasi fulani ulifanikiwa sana.

Rooney umeondoka ila umetuachia kumbu kumbu kubwa sana ya kuwa mfungaji bora wa Man United wa muda wote ukifuatiwa na Sir Bob Charton⚽⚽⚽

Hukua nyuma team ya taifa ya uingereza ukawa mchezaji bora kabisa na mfungaji bora wa kipindi chote..sio man u tu tutakaokukumbuka bali hata team ya taifa ya England wanakumbuka mchango wako mkubwa.

Rooney pamoja na mambo makubwa uliyoifanyia club ila nasikitika kukwambia ya kwamba hautajengewa sanamu na kupewa heshima inayostahili kama wanayopewa THE UNITED TRINITY japo wote wale umewazidi kwa mafanikio uliyoipatia man united.Hii yote inatokana na asili yako Rooney,wewe ulizaliwa Jiji la Liverpool na kukulia huko huko Liverpool na ukafanikiwa kuja kucheza soka katika jiji la Machester pale Theater of dreams na ukacheza kwa mafanikio makubwa kabisa.

Rooney kwa taarifa tu ni kwamba man u hawapo tayari kukujengea sanamu au kufanya tukio lolote lile hata mechi ya kukuaga kama tulivyomfanyia Ole Gunnar Solskjaer mwaka 2007 japo wewe ulikuwa bora zaidi yake

(kuagwa kwa Ole Gunnar Solskjaer)
Tukio kama hili Rooney usitegemee kabisa japo wewe ndio mfungaji bora wa club wa muda wote

UNITED TRINITY


Tuliwaaga kwa style nzuri kina Nick Butt,Giggs na wengine wengi sana ila kwako wewe haitawezekana maana wee ni mpinzani kwa kuzaliwa kwako Liverpool,haiwezekani kumjengea sanamu mpinzani wako hata sikumoja,labda ujue tu kuwa kuwa mfungaji bora na kumpiku Sir Bob Charton ambaye ni mmachester united halisi hadi kwa kuzaliwa, hukuifurahisha kabisa Man united japo ulifanya kwa moyo mkunjufu kuisaidia team.

Ila mioyoni mwetu tutakukumbuka sana Wayne Rooney

Kila lenye mwanzo halikosi mwisho,nakutakiwa maisha mema huko huendako.

Deadbody
 
Of course amefanya makubwa sana,, hata kama hataagwa Rasmi kama hao wengine but kumbukumbu(records) yake itadumu daima hadi ivunjwe na mwingine...... Goodbye Rooney....

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Kwa heri ya kuonana

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mapema sana mambo hayo ni mchakato to toka uhai wa club mpaka leo ni wachezaji watatu na kocha mmoja ukiacha best Denis law na Bobby nani mwingine yupo hapo? kumbuka pana ukumbi unaitwa Hall of fame umesema mapema ungesubiri wazza pana makubwa atafanyiwa kuuthamini mchango wake.
 
Tafadhali Tafadhali Tafadhali
Tufollow Instagram kama kandanda24 kupata updates za soka bongo na majuu
 
Kweli wewe the deadly body. Na je ikitokea akajengewa mkuu au kuagwa kiheshima ? Muwe na akiba ya maneno all the best wazza we will miss you alot at OT.
 
Hata kama hatoagwa au kujengewa sanamu ila RECORD YAKE ITAMLINDA

Lakini mbona umefanya mapema sana kuleta uzi kama huu ni jambo la muda tu utaongea
 
The United Trinity ni kina nani mkuu?

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Angestaafia united.

Binafsi sikuridhika alivyoondoka kwa style ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…