Kwaherini ndugu zangu wa JF

unaenda wapi? unahisi miez 7 inatosha, Yesu aliifanya kwa miaka 3
 
I hear your words, and while “get out” may sound harsh, I choose to leave in peace and without offense. The truth is, not every goodbye will be wrapped in kindness, but as for me, I will not repay sharpness with sharpness. As it is written, “Do not repay anyone evil for evil. Be careful to do what is right in the eyes of everyone... If it is possible, as far as it depends on you, live at peace with everyone” (Romans 12:17–18). So I go in peace, and may the Lord bless you abundantly my friend felakuti
 
Miezi 7 haitoshi lakini kuna wengine katika maeneo mengine ya dunia wana njaa na kiu ya haki inabidi niwapelekee pia chakula cha uzima
Huko kwingine wapo ana Timotheo, akina Priscilla watamaliza
 
Mdo 18:21
Lakini alipokuwa akiwaaga aliwaambia, “Nitarudi Mungu akipenda.” Akasafiri kwa meli kutoka Efeso.
Unaweza kuwa umedharau mbegu ya Imani uliyokuwa ukipanda ndani ya mioyo yetu hapa JF kutokana na maneno ya baadhi yetu lakini ukweli ni kwamba neno lile limeokoa maisha ya wengi zaidi ya walioona halina thamani kwao (kuna watu wanasoma na kuokoka pasipo kusema/kuandika neno).

Umetusaidia wengi, hupaswi kuacha sasa! Unapaswa kuendelea kutusaidia kukua na kuongezeka Imani! Upo hapa kwa sababu maalumu! Mungu amekuweka hapa kwa sababu. Badala ya kutii matakwa ya shetani yanayokutaka uache, ni bora ukaisikia sauti ya Mungu hivi leo na ukaitikia wito wake wa kuwahudumia watoto wake!

MAVUNO NI MENGI, WAVUNAJI NI WACHACHE!!!

Na wewe miongoni mwa WACHACHE ukituacha, nani kutuhudumia? Ulihubiri neno bila woga!
 
Sijaacha mkuu, naenda katika maeneo mengine yasiyofikiwa na Jukwaa hili. Yesu alituagiza twende ulimwenguni mwote, sio kuhubiri eneo moja tu. Lakini Mungu akinijalia nitarudi tena.👋🙏
Vizuri sana, piga kote kote mkuu, fanya kadri upatavyo nafasi
 
Marko 1:38
Yesu akawaambia, “Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo.”
 
Kitoto cha mchungaji baba ake karidhia kusilimishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…