Kwaherini wapendwa MMU

Kwaherini wapendwa MMU

nanjilinji

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
1,203
Reaction score
563
Kwa masikitiko makubwa naomba kuwaaga rasmi.

Naondoka hapa kwetu Njinjo kesho naelekea wilaya ya Liwale ambapo nimepata kibarua kwa mzee mmoja. Nijuavyo huko Mpigamiti hakuna Internet, hivyo haitakuwa rahisi kusoma makala nzuri za JF.

Hii imetokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa Kilwa na mfano ni hii (bofya). Mvua zimeathiri mashamba yetu na hivyo uwezekano wa kuendelea kuishi nyumbani wakati PESA ni shida inanilazimu nielekee Mpigamiti nikatafute kibarua. Naomba msamaha kwa niliowakwaza ingawa kwa upande wangu hakuna yeyote aliyenikwaza. Niliwapenda sana ila mafuriko yananifanya kwa moyo mzito nisepe. Kwa atakayetembelea huko tafadhali sana anitafute, Simu yangu ni 0754-235470.
 
Duu tembea uone hadi no umeweka ili uwanase wadada wa jf hatudanganyikiiii we nenda ukale samaki nchanga .
 
Tutakukosa sana mkuu nanjilinji kila la kheri huko uendako na kanafasi ka neti kakitokea tu usiache kuja kutupiamo hata kasalamu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom