Pre GE2025 Kwahiyo ni rasmi Machinga hamtaki tena utetezi bali mko na CCM kwa kila jambo?

Pre GE2025 Kwahiyo ni rasmi Machinga hamtaki tena utetezi bali mko na CCM kwa kila jambo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Tumesikia matamko huko Mwanza, Dar na kwingineko Viongozi wa Machinga na bodaboda kadhaa wakitoa tamko kuwa wao habari za maandamano hawazitaki na kuwa wanaunga mkono serikali na "juhudi" zake katika ustawi wao.

Well kupanga ni kuchagua, wameamua kuwa kwa sasa wako vizuri na utendaji wa serikali, halmashauri, polisi na migambo yake. Kwa maana hiyo wameula na hawana shida Tena na utetezi waliokuwa wanaupata wa bure ambao umesababisha wameheshimika.

Kama ni wote, maana hawajatokea wengine kukanusha basi hatuna sababu kuwapigia kelele wanapo lialia.
Bai Bai wamachinga na Bodaboda mtakula mlikopeleka mboga.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ni hasara kubwa sana kupoteza kutwa yako bure bure kipumbavu, tufanye kazi ndiyo njia sahihi ya kurahisisha maisha yetu katika ngazi zote za kifamilia.
 
Akina Nyerere walifanya kazi tofauti sana na hawa nyumbu and Co, never compare!
Kweli kabisa, kina Nyerere kama viongozi wa kitaifa "walifanya kazi tofauti sana na hawa nyumbu and co"
Leo Crocodiletooth umeongea kwa akili sana sijapata kuona. Nikweli hawa "nyumbu and Co" walio ikulu na pale Lumumba sio size ya kina Nyerere.
Umeeleweka kiongozi.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Bodaboda nao watu basi, hao machinga ndo kabisaaaaaa......🚮
 
Back
Top Bottom