Kwahiyo tutarajie kuwa waliopiga kura ya mapema leo, kesho hawatapiga kura ya Rais na Mbunge wa Muungano kwa sababu watakuwa 'busy'?

Duniahadaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
336
Reaction score
677
Nimesikia kutoka BBC kuwa Maafisa wa Uchaguzi na wanausalama wamepiga kura leo kwa sababu kesho watakuwa bize. Kumbuka kuwa kesho kutakuwa na uchaguzi wa NEC. Kwa hiyo tutarajie kuwa waliopiga kura ya leo ya mapema, kesho hawatapiga kura ya rais na mbunge wa Muungano kwa sababu watakuwa bize?

Naomba ujibu kwa utulivu.
 
Reactions: ffn
Hizo zinaitwa kura za watu wenye kazi maalumu.
Mwisho wa kunukuu.
 
Hii nchi ni kama tupo karne ya 16 huko...kuna mambo watawala na ccm wanafanya ....unashindwa kuelewa kama wanatumia kichwa kufikiri ama ni makalio...
 
Naomba kuuliza, mawakala walikuwepo? Je baada ya kupigwa zinahesabiwa leo au mpaka za kesho? Je zinalala wapi leo? Je zitalindwa na mawakala wa vyama vyote Hadi kesho?
 
Mwanakulitafuta, mwanakulipata, piga hao kama paka mwizi, ijumaa saa 7 mchana ndio tutaanza kuzungumza lugha ambayo tutaelewana.

Sirro amekwisha sema tii sheria bila shuruti. Wanakulitafuta msiwasikilize deko hao.

Piga wachakae, sisi tuna hitaji kuwa salama na nchi yetu hao waliotumwa na basha zao kina Ámsterdam tusiwasikilize wataharibu uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…