Kwako Amos Makalla kuhusu kamati ya kutatua migogoro ya ardhi Mabwepande

Kwako Amos Makalla kuhusu kamati ya kutatua migogoro ya ardhi Mabwepande

Cubana

Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
19
Reaction score
6
Kwako mkuu wa mkoa, ningependa kuzungumza na wewe kuhusu kamati yako ya kutatua migogoro iliyopiga kambi Mabwepande

Sidhani kama unajua kwa kina uhalisia wa hali ya huku kimazingira na haki za wakazi wa huku namna walivyozipata, kinachotaka kutokea wewe na ofisi yako ndiyo mtakuwa wahusika wa mwanzo.

Ni kwa makusudi kabisa kuna viashiria vya uvunjifu wa Amani, haiwezekani eneo ambalo Mahakama ilitoa hukumu watu waendelee na maisha yao na walioharibu mali wawalipe wananchi hao, na uhakiki ukafanyika na hao wahalifu walipewa muda wa miaka sita kukata rufaa hawakufanya hivyo tangu mwaka 2012, sasa iweje kamati yako itake wananchi waoneshe walipataje viwanja vyao wakati serikali ilishahakiki majina ya wamiliki wa viwanja na hili linakuja wakati tayari Serikali ilishachukua pesa za kuwekea mawe ya viwanja wananchi hao jumla wananchi walichanga mil 63.

Kesi hii Makonda anaiju, Happi anaijua.

Lutege anataka kutumia ukaribu wenu kuhalalisha maovu yake, anasema ana shamba la hekari 43 hivi Kinondoni kuna shamba la hekari hata 5? Watu 20 wanataka kupora makazi yenye nyumba zaidi ya 8000 yaani hekari 2000 ma zaidi, huku wakisema kwamba mwenye kutaka kuendelea kukaa ainunue tena ardhi hiyo kwa kuwa wao ndiyo wamiliki.

Je, Serikali ilifanya uhakiki na kuwapa wananchi "bango" yaani karatasi za umiliki wakati eneo hilo ni mali ya watu wengine?

Eneo ambalo Serikali imeleta huduma zote muhimu kama maji, umeme, shule na ofisi ya Serikali ya mtaa sasa unajiuliza hizi huduma Serikali ilileta kwenye mashamba pori kusikokuwa na watu, eneo lina soko sasa hili soko lipo porini kwenye mashamba?

Je, hukumu ya mahakama haina maana kwa kamati yako.?

Asilimia kubwa ya migogoro ya ardhi inatengenezwa na viongozi kwa kushirikiana na watu wenye uwezo kifedha. Huku kuna Lake oil na Ridhiwani ,wameleta mgogoro mkubwa sana hadi watu wamepoteza maisha yao

Kuna Mwamasika amempiga hadi mtu risasi hadi leo mtu huyo ni mlemavu.

Tunaomba Serikali kupitia Waziri wa Ardhi japo inasemekana ni wewe uliyowaahidi hao watu 20 kuwa watalitwaa eneo la Kinondoni nawe ukiahidiwa donge nono na hekari kadhaa

Mtasababisha machafuko.
 
Ndio maana hawa kina Makalla kuna kipindi walitiwa kwenye friji waziri wa ardhi anasemaje!
 
Mkuu poleni sana na hayo madhira ya kutengeneza ila nakushauri kitu kimoja tu.

Badala ya kugangaika na Makalla wewe kusanya documents zote muhimu toa copy nendanazo ofisini kwa Lukuvi uanze naye .

Huo mgogoro anaujua vizuri sana sasa huyo Makalla anataka kupiga noti kinyemela na watampatia kweli.
 
Ndio maana hawa kina makalla kuna kipindi walitiwa kwenye friji waziri wa ardhi anasemaje!
Wewe haya mambo yanayo hitaji kutumia ubongo kufikiri jaribu kuyakimbia maana siyo size yako.
 
Mkuu poleni sana na hayo madhira ya kutengeneza ila nakushauri kitu kimoja tu.

Badala ya kugangaika na Makalla wewe kusanya documents zote muhimu toa copy nendanazo ofisini kwa Lukuvi uanze naye .

Huo mgogoro anaujua vizuri sana sasa huyo Makalla anataka kupiga noti kinyemela na watampatia kweli.
Ili mradi tu nawe umesema!
 
Back
Top Bottom