Kwako boss

Qudabash22

Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
13
Reaction score
5
USHAURI WA AKIBA KWA OMOG.
Ubora wako ulithibitika toka ulivyokuja Tanzania pindi ulipokuwa unakinoa kikosi cha Azam(wana ramba ramba) na sasa bado unauthibitishia umma wa simba kwamba wewe sio wa nchi hii.
Unajua kutake risk as coach,Tar 25 february ulifanya substitution ambayo kila mtu aliinua mikono baada ya kumtoa beki wa kati na kumuingiza winga ambaye alikuja kuleta madhara makubwa sana na hatimaye karata zako ukazicheza vyema..nakusifu.
Ombi langu kwako kama Mwanasimba na mshabiki wa dhati wa klabu hii ya simba ni kwamba tunakuomba ujaribu mifumo tofauti tofauti katika mechi ya kirafiki ili timu yetu isizoee mfumo mmoja tu. Kocha wetu ni mpenzi sana wa mfumo 4-3-3 na 4-2-3-1..ni mizuri na umeweza kuimarisha sana safu ya ulinzi na kiungo.
Sasa nikiwa kama mwanasimba nakuomba kama kocha kujaribu kutumia mfumo ambao kwa sasa duniani hutumila kama njia ya kumshinda mpinzani. Mfumo huo ni mzuri sana hasa katika kujilinda,kushambulia na kutuliza timu.
Mfumo huo ni 3-4-3. Kikosi chetu ni kipana sana na kimesheheni vipaji mbali mbali na aina ya wachezaji ambao wanaweza kuutumia mfumo huu.
Sio kazi sana, mfumo huo unahitaji beki za kati 3 zenye speed na pace. Na sisi kwetu tunazo beki hizo ambazo ni JUUKO,MWANJALE NA BANDA JR. Ukiwasimamisha katika mfumo huo wataweza kutuletea kitu kipya zaidi. Beki hizi zinaweza kuzuia,kushambulia na hata kuuchezea mpira.
Ukija kwenye eneo la kati kati zinahitajika wing back mbili ambazo zinaweza kupanda na kushuka..na Kwa klabu yetu ya simba wapo watu hao..mfano kuna MOHAMMED HUSSEIN"TSHABALALA" ambaye anaweza kucheza kama wing bak ya kushoto pamoja na MZAMIRU YASIN ambaye anaweza pia kucheza kama wing back ya kulia.
Pia eneo la kiungo linabebwa na viungo wanaochezesha na kukaba pia..kwa timu yetu tunao aina ya wachezaji hao Kwa mimi nawapendekeza JAMES KOTEI na HAMISI NDEMLA.viungo hawa wanaungana na wing backs ya kushoto na kulia ilo kuweza kubalance timu. Unyumbulifu wao unaweza kuleta madhara kwa wapinzani.
Eneo la mwisho ambalo ni eneo la ushambuliaji litabebwa na Wachezaji wa 3 ambao ni KICHUYA,MAVUGO Na AJIB.
Hawa kazi yao itakuwa ni kuitumia mipira inayotoka kwa midifilders na kukwamisha kambani..
Pia wachezaji kama MKUDE,BOKUNGU,KAZIMOTO,LUIZIO,MOHAMMED IBRAHIM wanaweza sana kucheza mfumo huu.
Ukija uki"link" mfumo huu na Team za ulaya tunachukua Sample ya timu 2 ambazo ni CHELSEA na TOTTENHAM
timu hizi zimekuwa zikitumia mfumo huu kwa manufaa makubwa sana na hasa unadhihirika pale ambapo points,magoli ya kufungwa na kufunga kwa hizi timu.
Unaweza kuangalia wachezaji hao wa chelsea pamoja na wa Tottenham ukiwa link na wachezaji wa simba

Beki 3
Midifilder 4
Striker 3

Beki
Mwanjale-cesar-alderweireld
Juuko-luiz-dier
Banda-cahil-vertogen

Midifilder
Tshabalala-alonso-rose
Mzamiru-moses- walker
Kotei-kante-wanyama
Ndemla-fabregas-dembele

Striker
Kichuya-Pedro-delle
Mavugo-costa-kane
Ajib-hazard-eriksen


Huo ni mfano tu nimetumia kwa kublend timu mbili inayotumia mfumo huo...
Ni ushauri tu kwanza uanze kutumika katika mechi za kirafiki na ukionekana kuwa una manufaa basi mwakani "in shaa Allah" kwenye klabu bingwa kwa sababu kwa sasa hatuna sababu ya kuukosa ubingwa...
Naupongeza sana uongozi kwa kuhamasisha umoja
Nawapongeza sana mashabiki wa simba kuwa na umoja na nawasihi pia tuisapoti timu yetu ili tuweze kufikia malengo yetu.
VIVA SIMBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…