Mziwandawamama
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 1,303
- 939
Ujumbe huu ukufikie Christian Bella iwe unapita huku ama watu wako wa karibu wakufikishie ujumbe.
Mimi ni shabiki wako mkubwa sana tena sana nikiri wazi kwamba nakupenda sana kutokana na kazi yako nzuri ya uimbaji uliotukuka.
Pia nikuweke wazi nilizidi kukukubali wewe pamoja na kazi zako pale nilipojiridhisha kuwa wewe ni msanii unaejielewa kwa kutokuiga sijui niziite fasheni za kimagharibi kama vile kusuka nywele,kuvaa hereni,kukata nywele mikato isioeleweka nk.
Pamoja na kuwa hufanyi yote hayo lakini umebaki kuwa msanii mzuri mwenye mashabiki wa kutosha na kazi zako zinakubalika sana kaka Yangu.
Nikirudi kwenye pointi hivi majuzi nimeona picha zako za karibuni na kugundua wewe sio yule Bella wa miaka 3 iliyopita nyuma ambae alinikosha sana na kunifanya nimpende bure tu bila sababu yoyote.
Mdogo wangu Bella UNAJICHUBUA kama sio kutumia vipodozi vikali. Jambo hili limenifanya nipunguze credits juu yako na muziki wako pia.
Nafahamu hayo ni masuala binafsi lakini kwa kuwa wewe ni kioo cha jamii na jamii yenyewe ndio mimi sijapendezewa na hilo jambo.
Wewe ni mzuri sana mdogo wangu na rangi yako ni nzuri pia bila kutumia hayo makitu ya kubadilisha ngozi.
Asante,ni mimi shabiki wako wa ukweli#team bella.