KWAKO CHRISTIAN BELLA (King of the best melodies)

Mziwandawamama

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2015
Posts
1,303
Reaction score
939
Ujumbe huu ukufikie Christian Bella iwe unapita huku ama watu wako wa karibu wakufikishie ujumbe.

Mimi ni shabiki wako mkubwa sana tena sana nikiri wazi kwamba nakupenda sana kutokana na kazi yako nzuri ya uimbaji uliotukuka.

Pia nikuweke wazi nilizidi kukukubali wewe pamoja na kazi zako pale nilipojiridhisha kuwa wewe ni msanii unaejielewa kwa kutokuiga sijui niziite fasheni za kimagharibi kama vile kusuka nywele,kuvaa hereni,kukata nywele mikato isioeleweka nk.

Pamoja na kuwa hufanyi yote hayo lakini umebaki kuwa msanii mzuri mwenye mashabiki wa kutosha na kazi zako zinakubalika sana kaka Yangu.

Nikirudi kwenye pointi hivi majuzi nimeona picha zako za karibuni na kugundua wewe sio yule Bella wa miaka 3 iliyopita nyuma ambae alinikosha sana na kunifanya nimpende bure tu bila sababu yoyote.

Mdogo wangu Bella UNAJICHUBUA kama sio kutumia vipodozi vikali. Jambo hili limenifanya nipunguze credits juu yako na muziki wako pia.

Nafahamu hayo ni masuala binafsi lakini kwa kuwa wewe ni kioo cha jamii na jamii yenyewe ndio mimi sijapendezewa na hilo jambo.

Wewe ni mzuri sana mdogo wangu na rangi yako ni nzuri pia bila kutumia hayo makitu ya kubadilisha ngozi.

Asante,ni mimi shabiki wako wa ukweli#team bella.
 
We wawapi, unashangaa kujichubua kwa Mcongo?
Mkuu ni kweli wacongo waliowengi ndo zao lakini huyu kijana amejitahidi sana kudumu kwenye rangi yake muda mrefu kitu kilichonifanya nimpende zaidi lakini naona sasa ameshindwa na ameenza kuonyesha uhalisia wa vijana wa kikongo
 
Mkuu Wakongo bila kujichubua hawajioni kama ni 'mahandsome'. Muache tu aendelee naona sasa umekuwa kama utamaduni wao.Ngoja niendelee kula burudani....nani kama mama.......
 
Habari hii bila picha ya ushahidi inakuwaje lakini!?
Picha/video Muonekano wa Christian Bella juzi tu
Christian Bella alivyonogesha mkutano wa Magufuli, Mwanza
Source: MUHIDIN MICHUZI
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unashangaa Mkongo kujichubua mkuu?
Ongea mengine sio hilo,maana hatokuelewa.
Hiyo ndiyo 'identity' yao.
 
Weka picha za mnato tuone tofauti hiyo, isije ikawa lawama zisizokuwa na msingi
 
Mkongo na kujichubua ni kama Masai na Rubega.....akivaa suruali na shati na tai ndio unamshangaa.
 
Unauliza makofi central hahaha! Alafu wakipanda jukwaani wanaimba kiswahili kizuri wakihojiwa sasa,dah utashangaa wanajifanya hawakijui vizuri! Utasikia,wajuaa kwa ile mashooo nilipata mafaranga mingi sana,na ikinge nkaawacha kwa nyumba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…