Kwako Fundi

COBOL

Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
98
Reaction score
222
Fundi umekua ukijiongezea sifa mbaya sana kila majira yanapoenda. Kumekuwa na misemo maarufu kama "Fundi mkweli ni kinyozi tu", lakini hata hili sasa hivi si kweli. Kwanini na malalamiko yote haya huweki jitihada za kubadilika?

Fundi nimekupa order yangu ukaniahidi ndani ya siku saba itakua tayari. Fundi wiki ya pili sasa unanizungusha. Kwanini hujifunzi kwamba malalamiko yote haya yana athiri sifa na biashara yako? Jaribu kubadilika fundi

Amini kwamba pesa inarudi haraka kwa fundi muaminifu kuliko mwenye mizinguo. Unataka tukabane shingo ndo uelewe kwamba nina mipango yangu unanichelewesha? Au Unadhani nitarud tena kufanya biashara na wewe au mtu akiniuliza kama nina fundi mzuri wa kitu fulani nitamleta kwako?

Kwanini Unapoteza pesa zote hizi?

Kwa wenye biashara nyengine

Jaribu kuwa muaminifu kwa wateja wako. Kama haukuwa hivyo jaribu kubadilika uone namna milango itakavyo kufungukia kwa haraka kuliko ulivyowahi ona kwenye hiashara yako.

Unajua mteja unapomdhulumu kwa namna yoyote ile, iwe kwenye bei, huduma au ahadi za uongo huwa nafsi yake inaumia, kwanini mteja unae muumiza nafsi arudi tena kwako?

Wafanya biashara tujaribu kubadilika tuone matunda.
 
Mafundi bana sometimes wanazingua sana, kuna fundi cherahani nilimpa nguo yangu anirekebishie na pesa nikampa dah, alinizungusha huyo mda mrefu hadi nikasahau ni nguo gani niliyompa(suruali,sketi🤷‍♂️), siku ananipa nashangaa tu kumbe nilimpa suruali😀😀
 
Ni dharau tu zimewajaa, unakuta fundi yuko bize na cherehani kila siku, lakini nguo yako hashoni!
 
Ni dharau tu zimewajaa, unakuta fundi yuko bize na cherehani kila siku, lakini nguo yako hashoni!
Yaani, ilikua kila nikienda ananipa sound nguo yako iko tayari bado kitu kidogo tu hadi nikakata tamaa😀, fundi mwenyewe anaonekana mstaarabu yani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…