Ari Mpya Kasi Mpya, Ahadi ulituleteaJIBU KUTOKA IKULU
damu haimwagiki,na haki haitendeki
umekaa unataka HAKI?,utabaki kama MWALIMU na Chaki
mi ni maji we samaki,ila kihesabu ni buku na laki
mnachoongea siwasikii,niko bize naskiliza muziki (wa mipasho):biggrin:
Ari Mpya Kasi Mpya, Ahadi ulituletea
Vilevile Nguvu Mpya, Mbele Uliongezea
Ukweli Maisha Mapya, Kwako tulitegemea,
Chonde Chonde Mkuu, Mtaani ni Kugumu.
Mbona watutenga, nasi tulikuchagua,
Imani tulijenga, Daktari kutuagua,
Machozi yanilenga, Njaa yanikwangua,
Chondechonde mkuu, Mtaani Kugumu.
poleni sana
Mpoto alituma salamu, ukavunga ujazisikia
Roma akashika kalamu, nyimbo akakuandikia
We una akili timamu, sema tu hutaki zitumia
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?
Izzo-B akamtuma rizi1, Kaka umetukaukia
Nami naenda Mtandaoni, Jibu nasubiria
Natoa Yangu Maoni, Maisha Kulalamikia
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?
Maisha Magumu Jamani, au kwako wayaonaje?
Ntaabika Maishani, Sijui kesho Ikoje,
Nataabika Mtaani, Ahadi zako nizingoje
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?
hii tu ndio njia rahisi hamna nyinginenilishasema hadi kuchoka nchi hii nimeichoka,
mambo yanavyoendeshwa si kama tulipotoka,
kila nikifikiria machozi yananitoka,
sijui lini mtanzania anaweza kuokoka.
tukijipanga kwa ufanisi nchi tutaikomboa,
wala rushwa na mafisadi hakika tutawaondoa,
majumba yao ya kifahari nakwambia tutayabomoa.
tuijenge tanzania mpya wafilisi kuwachomoa.
mkuu the boss
kumbe hata huku huwa unapitia?
napenda mashairi
only ya siasa za kulalamika yananitia uvivu
nimewapa pole kwa kulia lia sana
mimi nilishaamua nitaishi as if nipo ugenini,mind my bussiness zaidi..
sitaki stress za siasa