Kwako Katibu Mkuu wa CCM ndugu Chongolo

Kwako Katibu Mkuu wa CCM ndugu Chongolo

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,875
Kwanza nikupe heshima yako, shkamoo na pole kwa majukumu makubwa ya kuongoza chama,

Siku kadhaa kabla ya sherehe ya uhuru ulifanya kikao na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya chama ndani ya miaka 60. Katika kikao hicho ulizungumza mambo mengi lakini kwangu napenda kuchangia kuhusu haya.

wakati ukimalizia kikao chako ulisema "unawashukuru sana viongozi ambao walipewa dhamana na viongozi ambao wanatuongoza sasa tukianza na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alianza baada ya uhuru kuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi yetu na baadaye mwaka moja baadaye kuwa rais wa JAMHURI WA TANZANIA na baadaye kuwa rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania na baadaye kumuachia kijiti mzee wetu alhaji Ali Hassan Mwinyi rais wa awamu ya pili". Nimeandika huu uzi baada ya kusikiliza nyimba, hotuba na matangazo ya watangazaji na washehereshaji SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA wakijaribu kutaja siku ya uhuru yaani tarehe 9 dec kama siku ya uhuru wa Tanzania bara.

Kwa heshima na taadhima Katibu mkuu ni vizuri nyie kama chama tawala mkatuongoza vyema kujua historia ya nchi yetu. Kwanza wakati Nyerere anakuwa waziri mkuu hakukuwa na Tanzania. Mwalimu Nyerere hajawahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania bali waziri mkuu wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika 1962 na baadaye Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwahiyosi kweli kwamba Mwalimu alikuwa rais wa kwanza wa jamhuri ya Tanzania kabla ya Muungano kama ulivyosema hapo juu.

Pili kuhusu suala la Tanzania bara hili halipo sawa, hakuna nchi inaitwa Tanzania bara iliyopata uhuru. Kwanini tunaogopa kusema Uhuru wa Tanganyika? au mnadhani itafanya Zanzibar ijisikie kutengwa? mbona Tanganyika ni neno fupi na rahisi kutamka kuliko Tanzania bara , shida iko wapi? tunamdanganya nani na hii Tanzania bara au tumeamua wenyewe kupotosha historia yetu?. Kama kuna sehemu panaitwa Zanzibar na kuna Tanzania visiwani basi kuna Tanganyika na Tanzania bara, wala tusiogope kusema na kujivunia. Neno Tanzania bara na Tanzania visiwani ni maneno yanayolezea position tu ya Tanganyika na Zanzibar kwamba moja iko kwenye nchi kavu na nyingine iko baharini haziwezi kuwa majina ya Mataifa haya mawili.

Jambo la tatu ni kwamba ulisema kwamba duniani kote baada ya uchaguzi chama kilichoshinda ndiyo huachwa kufanya kazi na kwamba vyama vingine hutulia kusubiri uchaguzi ujao. Namshuku Mungu sana mwenyekiti wako kakuumbua mchana kweupe kwamba mikutano ya vyama ni haki yao wala si hisani. Chama kikishachaguliwa kinaunda serikali, sasa kama siasa hakitakiwa ili kuacha serikali ifanye kazi wewe na viongozi wengine wa ccm huko mikoani mnafanya nini au nanyi ni viongozi wa serikali?

Mbele ya sheria CCM ni chama kama vyama vingine , kama shughuli za siasa hazitakiwa baada ya uchaguzi wewe kama katibu mkuu wa CCM onyesha hilo kwa mfano kwa kuacha kutembea huku na huko kukagua miradi acha viongozi wa serikali wafanye hizo kazi. SIJUI BAADA YA RAIS KUSEMA MIKUTANO NI HAKI YA VYAMA BADO UNAENDELEA NA MSIMAMO WAKO WA DEC 8 AU UMEFUNIKA KOMBE!

Nchi hii ni yetu sote bwana, tutende kwa haki.
 
Back
Top Bottom