Kwako Liberian girl

Kwako Liberian girl

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Umekua kama tui la nazi kwenye penzi hili!, utamu wako ni kama hewa laini inayopuliza wakati wajoto.

Nikianza na ngozi yako nitamaliza na umaridadi wako!, unaponivutia zaidi ni pale unaposema unapenda upekupeku!.
Haha! kama ni tunu nimepata na kama ni nuru hakika unaangaza.

Si kwa miguno na michuchumio wala si kwa ajizi na makadirio, unanipa vitamu bila kipimishio!.
sikutangazi kwa vijizi, maana wao kukupata mpaka kwa nguvu za hirizi!.
kuna wanaojiita "maradona" ati wanafunga magoli kila kona!, wamesahau ujuzi wa mkufunzi unapita weledi wa wanafunzi!.

Mimi sifungi kila kona, ila najua magoli yangu wayaona yanapita kwa nyavu, nasifungi kwa mkono ila kwa kiungo kilichonona!.

Natamani nianzie dodoma ila singida hakika pamenona!, unanifanya niumwe sonona kwa hizo nywele za kibantu na ngozi iliyopikwa kwa nazi na sio koroma!.

Mshairi wangu alinifunza "nisianze na moja ila mbili!", Wewe ukanikuza nisipige kimoja bali viwiliviwili!. Haha!

Nashukuru nimekuwa kenzy, sio wa mapambio bali mjuzi wa utenzi mwenye kuenzi lako penzi!.

kwako Liberian girl..
 
Mkuu mashairi yako yanashabiana mno na kitabu cha wimbo ulio bora , nilishang'oa mchuchu kwa wale wa shalom shalom kwa hayo mashairi master😊
Haya yangu hayatoki huko, haya yameratibiwa kwa hisani ya bubujiko la penzi toka kwenye vilindi vya penzi mbonyeo,mbinuko na muinuko!.
 
Back
Top Bottom