Kwako Mkuu wa Wilaya ya Mwanga - Kilimanjaro

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Salamu sana. Na baada ya salamu je hujambo? Mimi sijambo kabisa.

Dhumuni la waraka huu ni kukupongeza kwa utendaji kazi wako. Ilikuwa jana 24/8/2017 ambapo katika mojawapo ya kijiji cha wilaya ya Mwanga wakazi wake walifanya kosa la kulisha mifugo kwenye eneo jipya ambalo serikali imeamua liwe hifadhi.

Mifugo yao ilikamatwa kwa kosa hilo. Kinachonifanya nikusifu Mkuu wa Wilaya ya Mwanga ni pale ulipofika eneo la tukio, ukaamua mgogoro huo ambao ulifanya maamuzi ambayo ni FAIR, hukuwapendelea wale wenye mifugo na wala hukuipendelea serikali, ulihakikisha haki inatendeka kwa pande zote mbili. Ahsante sana.

Nakuomba upange ratiba yako ya ziara uje hapo kijijini uongee na hao wananchi lakini katika masuala utakayoongea nao mojawapo uwakumbushe utunzaji wa mazingira na pia kuwasisitiza kuwa kuna maeneo ambayo hawaruhusiwi kulisha mifugo yao.

Kama uko JF utasoma huu ujumbe wangu, kama hauko hapa naamini kuna wapambe wako watakupa salamu zangu, na hata bosi wako mama Anna Mghwira yumo humu JF.

Ahsante JPM kutuletea jembe wilaya ya Mwanga, ila sasa nakuomba kale "kamsuguano" kako na DAS wako mkamalize ili muweze kusimamia vema wilaya ya Mwanga.

Sina mengi kwa leo, kalamu naweka chini

Wako mtiifu,

NAHUJA
mzaliwa wa kijiji hicho
 
Viongozi wanapofanya vizuri wanastahili pongezi
 
Viongozi wanapofanya vizuri wanastahili pongezi
Ni kweli chakii, jana kanifurahisha maana sikutegemea kuwa hawa wateule wa mkulu wanaweza kufanya maamuzi mazuri bila kuumiza upande mmoja.
 
sasa si ungesema hapa hiyo haki katendaje mpaka ukampa bichwa lote hilo? La sivyo ungemuandikia barua kisha ukapeleka nyumbani kwake, lakini kama unaleta jambo hapa lazima useme kiunagaubaga kwamaana wengine wala hatujui hiyo wilaya iko wapi.
 
Umeuliza vema, GIUSEPPE, ni kwamba kwenye huo mgogoro alifanya maamuzi ambayo hakuwaumiza wale wafugaji na wala hakuiumiza serikali (kama inaumia). Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro. Karibu sana Mwanga - Kilimanjaro
 
Hujajibu kitu, umekopi maneno yaleyale, sema alifanya nini na sisi wakuu wa wilaya wengine tujifunze hapo.
 
Wapare bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…