Mkuu, mke wa mtu ni simu.
Uchungu wa kusalitiwa usikie kwa mtu tu.
Halafu nimeokoka sasa.
Salama baharia? Nakuona kwenye tasnia yako
Yaani stori nzima ipo episode 2 lakini mwamba naona kama anaikaushia hivi...
mkuu watu wakishaoana mahaba yanapungua,nimechunguza hili jambo.Labda kama anapewa ndogo na huyo dada wa saluni. Ila vingine vyote anaweza kuvipata kwa mkewe
Karibu.Ahsantee
Umeanza vizuri lkn ukaharibu mwishoni [emoji2]Na wanawake huwa hawana kaba/usiri...unapotoka nae ni lazima atangaze mahusiano yenu ya siri kwa marafiki /mashoga zake ambao kwa asilimia kubwa nao huwa ni masnitch zake. Hivyo kunakuwa hakuna usiri tena. Huyo jamaa nae ni fala alishindwa nini kujisogeza hata bwagamoyo au mji kasoro bahari alafanye yake kisha arudi dar. Dar ni ndogo sana kufanya huo upuuzi
Hakika.Jambo hili sio jema kabisa. Hapo hata jamaa aombe MSAMAHA Bado dada maumivu yatakuwepo
Umenilisha maneno mkuu [emoji2]. Sikusema nataka nimjue kabla ya ndoa.Lakini we jamaa si ulisema unamchumba mchana Mungu ila Kwa kutokumjua Lowasa ukaona kama ana exposure ndogo? Hiyo sio point yangu
Kwenye ule Uzi, ulisema Binti anagoma kabisa kukupa Hadi ndoa ifungwe, inamaana wewe ulikua inahitaji ujipooze sahihi? Sasa huu ulokole wa kutaka kujipooza kabla ya ndoa ni version ya wapi?
Hausafishi mtambo Kwa kuwa mlokole au umeamua tu uachane na mambo ya ujana?
[emoji23][emoji23] dah!Yaani stori nzima ipo episode 2 lakini mwamba naona kama anaikaushia hivi...
[emoji23][emoji23]Naona unapiga paparara tu hapa
HUjui ndoa wewe
Usihukumu kabla hujasikia stori upande wa pili
Usikute kijana wa watu anakaa miezi 2 ndo anachangamshwa
Cha kufia nini ngoja aende arusha [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]Inafanyiwa filtering
[emoji848][emoji848]mkuu watu wakishaoana mahaba yanapungua,nimechunguza hili jambo.
na ndoa nyingi zinakufa chini ya muda walipokua na mahusiano.
wananyanduana kwa miaka mitatu wakiingia kwenye ndoa mwaka mmoja tu wanaanza kutimuana,kugombana mpaka ndoa inakufa.
kataa ndoa wanazidi kupata nguvu.
Mapenzi sio ya kuchukulia serious, utakufa mapema. Ona sasa miaka 30 una BP, na hizo dawa huwa zinaua Figo. Jaribu kufanya mazoezi na ku focus na mambo mengine ili uachane na hizo dawa kwani umri bado no mdogo.Mapenzi shwain nlijitia kupenda nikaambulia high BP nikiwa na miaka 30 hadi leo natembea na mafuko ya dawa kama mwathirika nangoja kupata mshituko tu nakata kamba naacha vitoto vyangu vidoooogo😏
Tatizo ni mazoea. Ni kama kununua gari jipya, unakuwa na mchecheto nayo baada ya muda unaona ya kawaida sanamkuu watu wakishaoana mahaba yanapungua,nimechunguza hili jambo.
na ndoa nyingi zinakufa chini ya muda walipokua na mahusiano.
wananyanduana kwa miaka mitatu wakiingia kwenye ndoa mwaka mmoja tu wanaanza kutimuana,kugombana mpaka ndoa inakufa.
kataa ndoa wanazidi kupata nguvu.
Polo ya Blue?Naishi Dodoma ila kwa sasa nipo Dar Ukonga KMKM ambapo nimejenga makazi yangu ya kupangisha. Kama mna kumbukumbu nzuri nilileta uzi humu majuzi nikiomba ushauri wa namna ya kudeal na mpangaji wangu mmoja mjeda aliyetaka kunidhulumu kodi na wadau mkanipa ushauri murua kabisa na j3 naenda kulipwa pesa yangu.
Nikiwa naingia KMKM recreation centre kwa miguu, getini ikanipita gari aina ya Volkswagen polo kwa kasi ikiendeshwa na binti mmoja mlimbwende. Nilivyofika ndani nikamkuta bidada analia kwa uchungu, wahudumu na wateja wengine wakawa wanamshangaa! Akaagiza chupa ya wine. Nikawa namu-observe kwa takribani nusu saa. Baadaye nikamuita dada aliyemuhudumia na kukwambia nitalipia ile chupa ya wine. Mhudumu akaenda kukwambia ila dada hakujibu chochote.
Akaonekana amenipuuza na kuendelea kunywa ile wine kwa kasi. Baada ya dk 20 hivi, nikiwa nimeinamia simu yangu yule dada akahamia mezani kwangu! Tukasalimiana, akaomba kukaa nikamruhusu, kabla hajaanza kujieleza nikamwambia asubiri, nikamsihi aendelee kulia ili uchungu umtoke moyoni.
Aliyonieleza baada ya kumaliza kulia yanaogopesha. Anadai mume wake amebadilika sana, anatembea na binti mmoja wa saluni ambayo iko jirani na nyumbani kwao. Jamaa ameaga anaenda safari ya kikazi, baada ya mwanaume kupaki begi la safari, mkewe (ambaye ndio huyu dada) akakuta pair ya viatu vya kike na iphone full boxed, mkewe alikuwa anamuwekea mumewe makoti ya baridi kwasababu jamaa aliaga anaenda Arusha, wakati mkewe anaweka hayo Makoti jamaa alikuwa ametoka.
Jamaa alivyorudi mke akanyamaza. Jamaa akaondoka leo asubuhi mkewe anamuangalia tu. Sasa mchana huu huyu dada akiwa na mawazo saluni akakutana na shosti yake, shosti mtu bila kujua, akamwambia huyu dada kwamba kakutana na mume wa huyu dada Mlimani City akajaribu kumsalimia lakini shemeji mtu hakumuona wala kumsikia. Mke mtu akatoka nje ya saluni akampigia mumewe akajifanya yeye ndio kamuona, mwanaume akaanza kujikanyaga! Akazima na simu (inaelekea anajipanga kudanganya zaidi).
Kumbe baadhi ya wanawake wa pale saluni wanajua jamaa anatoka na hako kabinti ka saluni na kabinti hakakuwepo leo!!! Wafanyakazi wenzake pale saluni wakasema walikuwa wanashindwa kumwambia wakihofia kuonekana wafitini! Mke kaunganisha dots kagundua kwamba ndio maana jamaa alikuwa na pair ya viatu na simu mpya!!!
Mkuu, umeharibu huku. Kama upo JF kakiri tu kwa mkeo wala usiendelee kudanganya.
Dada kalewa sana hapa, ingekuwa enzi zangu kabla sijaokoka leo pangechimbika.
Kanipa funguo za gari na handbag yake. Sijui anapoishi ila anasema akilewa sana nimtafute bodaboda anaitwa ......hapa nje ya KMKM atanielekeza kwake.
Sisi wanaume sijui tumerogwa na nani. Mwanamke mzuri hivi, msomi, mchapakazi, halafu anasalitiwa kindezi namna hii [emoji22]
NGOJA iendelee kunyesha tuone panapovuja ..
Sawa mkuu.Usimsaidie mke wa mtu, uisimuonee huruma mke wa mtu,
mambo yao ni juu yake na mume wake.
Unaweza ona unamsaidia kumbe unamuongezea matatizo.
Pole inatosha, kubeba handbags na funguo za watu za gari ni kujiingiza kwenye matatizo ya watu.
kama unamtaka acha wamalizane na mumewe waachene ndio mbebane sio kubeba ubaba huruma kwenye mambo ya watu.