Kwako Rais Samia kuhusu uhamisho wa mtoto kutoka shule binafsi kwenda ya umma

Kwako Rais Samia kuhusu uhamisho wa mtoto kutoka shule binafsi kwenda ya umma

Adabwash

Senior Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
101
Reaction score
216
Kwa Heshma na Taadhima Nakuandikia ili Ufahamu kero inayowakumba baadhi ya watu katika Mada tajwa hapo juu

Ninaye mdogo wangu kutokana na mazingira aliyokuwa nayo Alipelekwa shule binafsi mpaka alipomaliza KIDATO cha pili na kufanya mtihani wazazi wakayumba kimaisha na kupelekea kutokuweza tena kumudu kumsomesha provate schools

Mzazi Kaenda Kumuombea Mtoto Shule ya Karibu ya serikali ila Mwalimu Mkuu Akamjibu kuwa kwasasa serikali haifanyi tena UHAMISHO WA mwanafunzi kutoka private kuingia serikalini,

Mzazi Ameenda wilayani Mkuranga kujaribu kuona kama changamoto hiyo itapatiwa ufumbuzi ila DAS WA wilaya Akamjibu kuwa wao kama wilaya hawatoweza kulifanyia Kazi kutokana na hizo kanuni za serikali,

Mzazi Akatafuta namba ya Waziri WA Tamisemi ndugu Mchengerwa,Akampigia simu kumuelezea naye kwaharaka haraka Akamjibu kuwa kuwa Hajui kama Itawezekana kwasababu mzazi alimpeleka mwenyewe Mtoto huko private school,

Sasa Swali linakuja je hivi NI sahihi MH RAIS Kwa serikali yako Kufunga kanuni ambazo zinashindwa kuzingatia ya Kuwa Kuna VIFO Kwa wazazi au walezi ambao wabawasomesha watoto wao private schools na kwamba likitokea hilo la mungu watoto hawa watahitaji Kurudi Public schools

Au Pia Kanuni zinashindwa kujua kuwa pia Kuna Kuanguka Kimaisha Kwa Mzazi na kupelekea kutoweza tena Kumudu gharama za private schools na kuhitaji Kurudi public schools?

Au serikali imezingatia vigezo gani hasa mpaka wakaweka Kanuni hizi?

Au ndo NI mwisho WA elimu ya Mtoto ikiwa Kwa Namna yeyote Ile imeshindikana kuendelea na private schools?

Mtoto wetu tangia shule ifunguliwe yupo nyumbani sababu wazazi wamekosa Ada na serikali imeshindwa kumpokea,na mwaka huu ikitakiwa aendelee na KIDATO cha tatu,

Ahsante
 
Kwa namna wabongo walivyo na roho mbaya,hapo wanafurahi nakuona wanamkomoa mzazi.

Hizo kanuni hutungwa na watu wamekulia maisha ya dhiki,wamedumaa,chuki imewajaa.

Tena huyo mtoto akifanikiwa kuhamia hapo atakutana na bullying kutoka kwa walimu kwa huo uhamisho wa kutoka Private.
 
Nafasi yake alipewa mwingine baada ya kutorepoti shule ndugu mzazi
Endeleeni kujichanga mtoto amalize elimu yake
Unahisi kuna mzazi Ambaye hataki kumsomesha mwanaye Kwa makusudi? Je ikiwa mzazi au mlezi au sponsor wamefariki? Unayazungumziaje hayo?
 
Nafasi yake alipewa mwingine baada ya kutorepoti shule ndugu mzazi
Endeleeni kujichanga mtoto amalize elimu yake

Nafasi yake alipewa mwingine baada ya kutorepoti shule ndugu mzazi
Endeleeni kujichanga mtoto amalize elimu yake
Kumbuka kuna mpk Mtoto wakike kapata mimba,akaachwa akazaa na bado akarudi shule,kwann hawa wengine wasipewe mlango WA dharura?
 
Hio system ipo tangu zamani. Labda waifanyie mabadiliko
 
Back
Top Bottom