Kwako Waziri wa Mambo ya Ndani

Kwako Waziri wa Mambo ya Ndani

Halaiser

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
4,230
Reaction score
6,653
Nianze Kwa kusema au kuuliza kuwa hivi huyu Waziri husika yupo kweli na kama yuko kasusia awamu hii ya sita au?? Kwenye awamu ya tano alisikika Sana akikemea mwenendo mbovu wa Jeshi la Polisi hasa kitengo cha Usalama Barabarani. Sasa hivi kimya.

Kero yangu kubwa ni hili suala la sticker baada ya ukaguzi wa gari. Kwa magari madogo ya binafsi sticker imeandikwa Tsh 3,000/- lakini wanakuambia utoe sh 5,000/- hadi sh 7,000/-.

Na Kwa magari ya biashara imeandikwa Tsh 5,000/- lkn unaambiwa utoe sh 7,000/- Hadi sh 12,000/- . Je ukweli uko wapi?

Hata kama uko tayari kuwapatia wakati mwingine inakuwa kero kwani wanakuzungusha nazo sana. Mara zimekwisha au Vehicle Inspector hayuko yuko Barabarani utakutana nae huko. Huko Barabarani wanakukamata Kwa kutokuwa nayo na kukuandikia fine.

Hebu wahusika liangalieni hili.
 
Simbachawene hakustahili kuwa Waziri wa hiyo Wizara, kapwaya na kapoa sana. Hii Wizara inahitaji mtu mgumu na mwenye uelewa mzuri wa masuala ya vyombo vya ulinzi na usalama. Katika mataifa mengine ndiyo maana wanawekwa MAJENERALI wa majeshi.
 
Ndiyo maana nikauliza yupo ama kasusa. Kapoa mno hata Naibu wake nae vivyo hivyo. Utafikiri hawapo.
 
Yani mtu anakuwa Boss wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto halafu hana any wasifu wa kulidhisha kwenye nyanja ya ulimwengu wa ulinzi na usalama! Magu alifanya uteuzi kwa kuwaonyesha baadhi ya watu kwamba ukitemwa ukakaa kimya basi unaweza kuteuliwa tena. Ulikuwa ni ujumbe kwa waliotenguliwa kisha wakawa 'wanawashwa washwa' kukosoa.

Simbachawene hana wasifu wa kukalia kiti cha hii Wizara kabisa.
 
Ndiyo maana nikauliza yupo ama kasusa. Kapoa mno hata Naibu wake nae vivyo hivyo. Utafikiri hawapo.
Yupo sana, hivi vyombo chini ya Wizara yake VIMEOZA na hana uzoefu wala uelewa wa nyanja za Ulinzi na usalama. Hao wote ni rahisi sana kuwa compromised and manipulated katika utendaji wao.
 
Mnamuonea Simbachawene. Huyo ni kivuli tu hana mamlaka yoyote.
IGP anaripoti direct kwa Samia
Kamishna magereza na uhamiaji hivyo hivyo.
Muulizeni kilichomkuta Lugola na misifa yote ile.
 
Hii inapaswa iwe taarifa kumpa Ndugu Waziri. Waziri hawezi kujua kila kitu kama hiki kwamba labda umepigwa bei ya stika. Wakati mwengine tuwasaidie taarifa viongozi siyo kila mmoja anaweza kujua kila kinachoendelea mitaani.

Kuna Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchi nzima. Halafu Waziri si juzi alikuwa na Rais Arusha haya mengine yanatoka wapi?
 
Sisiyemu nafikiri ni mateso tuliyoshushiwa watanzania. We fikiria mtu unakadiriwa kodi kabla hujaanza kufanya biashara. Passport unaambiwa gharama ni laki na nusu ila ukifika inapinduka zaidi.
 
Hii wizara inabidi igawanywe mara mbili,wizara ya polisi(ulinzi wa raia na mali zao etc etc);wizara ya mambo ya ndani(uhamiaji na uraia) ,na futilia mbali mawizara tusiyoyahitaji nchi hii inahitaji wizara 15 tu.tuendelee kulalama humu
 
Hii inapaswa iwe taarifa kumpa Ndugu Waziri. Waziri hawezi kujua kila kitu kama hiki kwamba labda umepigwa bei ya stika. Wakati mwengine tuwasaidie taarifa viongozi siyo kila mmoja anaweza kujua kila kinachoendelea mitaani.

Kuna Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchi nzima. Halafu Waziri si juzi alikuwa na Rais Arusha haya mengine yanatoka wapi?
Mkuu naulizia ukimya wake ktk kutatua kero zinazohusu Wizara yake. Mkono wa Serikali ni mrefu kuliko wa Taasisi yeyote ile. Halikadhalika masikio yake yanasikia zaidi ya wengine. Vivyo hivyo pua yake huweza kunusa zaidi. Hivyo naamini haya yote ameyapata lkn bado yuko kimya.
 
Sawa ndugu. Naamini Waziri wetu atapata hii taarifa.
 
Back
Top Bottom