Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
HUU SIO MTONGOZO, ni neno la kuhusudu(word of admiration) kwa mwanamke ambaye nimekua nikifatilia michango yake humu JF MMU kwa takriban miaka mitatu kabda na baada ya mimi kua member wa blog hii. Nimefatilia michango ya weengi sana kwa muda huo lakini huyu katengeneza picha fulani akilini mwangu kwa consistence ya discipline ya michango yake.
Namzungumzia Emmyta. Picha niliyoijenga kwake ni dada mpole, mwanamke mcheshi, binti mwenye nidhamu ya kike hasa, asietaka makuu wala magomvi na mtu. Kwa kusoma michango yake nimemuumba katika fikra zangu mwanamke mtulivu anaechagua maneno na mwenye kujitambua.
Emmyta hamkwazi mtu, Emmyta hashushuani na mtu, Emmyta hamtukani mtu hata akichokozwa, Emmyta kama alivyo kunguru mwoga hukimbiza ubawa wake pale kwenye makabiliano ya maneno. Ukimkera Emmyta kwa maneno na ukachelewa kumuomba radhi basi atakuomba radhi yeye! Emmyta umelelewa ukaleleka wee dada
Uchaguzi wa Avater yake iwe ni picha yake yeye mwenyewe au sio yake ni miongoni mwa vitu vilivosaidia kumpa manyota yote haya. Avater ya kuonyesha bashasha na tabasabu la furaha, uchangamfu, upole, mapenzi na heshima. Haya Emmyta hebu njoo huku, kaa hapo, inua mikono juu nikuombee dua Emmyta, kisha useme Aamiin, na dua ya sisi wahenga hua haidondoki na hairudi nyuma asilani
Mungu Akupe kila la heri Emmyta, Mungu Akulinde na kila la shari, Akunusuru na husda za mahasidi Emmyta, Mungu Azidi kukujaza mapenzi kwa watu wote, wadogo kwa wakubwa. Mungu awabadilishe maadui zako wawe marafiki zako
Emmyta, kama hujapata mume Mungu Akupe mume mwema mwenye kheri na wewe.
.Emmyta kama una mume Mungu awape masikilizano na awajaze mapenzi kati yenu.
Awajaalie watoto idadi mnayoitaka na Awape rizki halali, yenye wasaa(nyingi) na yenye kuendelea
Kwa wale wanaounganana na mimi katika kumpa manyota haya Emmyta hebu nisindikizeni kwake kwa kugonga like nyingi iwe ishara ya kumzawadia Emmyta, aendelee na moyo huohuo