Kwako wewe dada ninaye kuhusudu/ku admire MMU

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
HUU SIO MTONGOZO, ni neno la kuhusudu(word of admiration) kwa mwanamke ambaye nimekua nikifatilia michango yake humu JF MMU kwa takriban miaka mitatu kabda na baada ya mimi kua member wa blog hii. Nimefatilia michango ya weengi sana kwa muda huo lakini huyu katengeneza picha fulani akilini mwangu kwa consistence ya discipline ya michango yake.

Namzungumzia Emmyta. Picha niliyoijenga kwake ni dada mpole, mwanamke mcheshi, binti mwenye nidhamu ya kike hasa, asietaka makuu wala magomvi na mtu. Kwa kusoma michango yake nimemuumba katika fikra zangu mwanamke mtulivu anaechagua maneno na mwenye kujitambua.

Emmyta hamkwazi mtu, Emmyta hashushuani na mtu, Emmyta hamtukani mtu hata akichokozwa, Emmyta kama alivyo kunguru mwoga hukimbiza ubawa wake pale kwenye makabiliano ya maneno. Ukimkera Emmyta kwa maneno na ukachelewa kumuomba radhi basi atakuomba radhi yeye! Emmyta umelelewa ukaleleka wee dada

Uchaguzi wa Avater yake iwe ni picha yake yeye mwenyewe au sio yake ni miongoni mwa vitu vilivosaidia kumpa manyota yote haya. Avater ya kuonyesha bashasha na tabasabu la furaha, uchangamfu, upole, mapenzi na heshima. Haya Emmyta hebu njoo huku, kaa hapo, inua mikono juu nikuombee dua Emmyta, kisha useme Aamiin, na dua ya sisi wahenga hua haidondoki na hairudi nyuma asilani

Mungu Akupe kila la heri Emmyta, Mungu Akulinde na kila la shari, Akunusuru na husda za mahasidi Emmyta, Mungu Azidi kukujaza mapenzi kwa watu wote, wadogo kwa wakubwa. Mungu awabadilishe maadui zako wawe marafiki zako

Emmyta, kama hujapata mume Mungu Akupe mume mwema mwenye kheri na wewe.
.Emmyta kama una mume Mungu awape masikilizano na awajaze mapenzi kati yenu.
Awajaalie watoto idadi mnayoitaka na Awape rizki halali, yenye wasaa(nyingi) na yenye kuendelea
Kwa wale wanaounganana na mimi katika kumpa manyota haya Emmyta hebu nisindikizeni kwake kwa kugonga like nyingi iwe ishara ya kumzawadia Emmyta, aendelee na moyo huohuo
 
Mkuu karudie tena kusoma saikolojia kabisa

Maana watu wapo tofauti KBS

Mfano Mimi nina kaundishi kakali kenye kuudhi hii nilianza nikiwa secondary watu wakiona maandiko yangu yaani wanadhani mm ni jitu kubwa la kutisha sana ni jeuri nisiyekamatika yaani kifupi wananiogopa sana nyaraka zangu


Lkn ukija kihalisia Mimi ni kinyume kabisa ya fikiria za watu

Hivo nakuambia fikiria yako uliyoiweka kwa mtu huyu ipindue iwe kinyume


Teh
 
Inawezekana wewe unadhani upo tofauti na unavojionyesha katika maandiko yako, lakini watu wengine ndio wanakuona na wako kwenye nafasi nzuri ya kuelezea tabia zako kuliko kuji asess mwenyewe
 
Kwaio unatak kutuaminisha kuwa emmyta hastahili sifa hizo zote
 
Inawezekana wewe unadhani upo tofauti na unavojionyesha katika maandiko yako, lakini watu wengine ndio wanakuona na wako kwenye nafasi nzuri ya kuelezea tabia zako kuliko kuji asess mwenyewe
Yaani kama umesoma vzr Niko kinyume kbs na nyaraka zako kitabia walioniona na kukaa nami au wale walioona mabandiko yangu baadaye kukaa nami ktk uhalisia hudecre kbs kuwa walivokuwa wakinifikiria siyo kbs tokana na maandiko yangu


Teh
 
Yaani kama umesoma vzr Niko kinyume kbs na nyaraka zako kitabia walioniona na kukaa nami au wale walioona mabandiko yangu baadaye kukaa nami ktk uhalisia hudecre kbs kuwa walivokuwa wakinifikiria siyo kbs tokana na maandiko yangu


Teh
Hapa hatuzungumzii maandiko na story za kutunga kama hadithi, nimemfatilia huyu dada michango yake katika nyuzi tofauti zenye maudhui tofauti na kuna consistance(mfanano au muunganiko) katika tabia ya uandishi na reactions zake kwa vichocheo mbalimbali
 
Duuh! Nimejikuta nasoma mara tatu tatu pasi kuamini mijisifa uliyonimwagia hapa.

Nikushukuru tu Kaka kwa kuliona hilo kutokana na maandishi na hiyo Avatar ya Emmy. Ahsante sana dua zako nimezipokea Amiin.

Ubarikiwe Mkuu. [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Mungu Azidi kukubariki leo, kesho na siku zote....Aamin
 
Dua kupokelewa manake maombi yamepokelewa mkuu
 
Mkuu sema tu umempenda emmyta ungependa umuone karibu yako for the rest of your life
Hahahaa mkuu, mi ni mwanaume na Emmyta ni mwanmke, hakuna ajabu mimi kumpenda na kutongoza lakini nimeweka wazi toka mwazo kua hili halikua tongozo ni maneno ya kum admire tu, kuna ubaya katika hilo mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…