Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
Mwanaume mmoja mkazi wa Kibundani katika Kaunti ya Kwale nchini Kenya amefariki dunia baada ya kupigwa na kundi la watu wakimtuhumu kuwa na Coronavirus. Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo.
=====
KENYA: MTU MMOJA AUAWA NA RAIA KWA KUDHANIWA ANA #COVID19
Polisi huko Kwale wanakisaka kikundi cha watu ambacho kimemuua kijana Hezron Kotin eneo la Kibundani baada ya kumtuhumu kuwa na #COVID19
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Msambweni, Nehemia Bitok alisema kijana huyo alikuwa akitembea kutoka kwa eneo la kunywa na aliingia kwenye kundi la vijana ambao walianza kupiga kelele kuwa ana ugonjwa
Vijana hao walishambulia mtu huyo wakiwa na silaha na kupelekea kifo chake. Kamanda wa Polisi alisema, waligundua jeraha kubwa kichwani mwake na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Msambweni
Polisi wameonya raia dhidi ya kuchukua Sheria mikononi mwao au kutoa madai ya uongo wakati Nchi inachukua hatua za kupambana na janga la #COVID19
Kaunti ya Kwale imeanza kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Afya juu ya kushughulikia kuenea kwa virusi hivyo. Afisa Mkuu wa Afya, Juma Mbete alisema wameweka vituo vitano vya kutengwa katika Kaunti zote tano