Uchaguzi 2020 Kwamba Watanzania wenye njaa wanahitaji tamasha la kuchambua wasanii wakupiga kampeni?

Uchaguzi 2020 Kwamba Watanzania wenye njaa wanahitaji tamasha la kuchambua wasanii wakupiga kampeni?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nchi hii watu wanaleta dharau, chama chetu tawala kinaleta dharua kubwa kwetu.

Awali tuliambiwa hakuna haja ya wasanii, mara paap upepo umegeuka tumeamua kufanya tamasha la wasanii tuchuje nyimbo za kuimbwa kwetu wapiga kura?

Je, ndipo mawazo na fikra zetu kuhusu kuvutia wananchi zilipoishia? Kwamba watu wakamwangalie diamondi ili wapate mlo wa siku? Wakamwangalie masanja wapate ada za watoto? Wakamwangalie Mpoto wapate fedha yakulipa Kodi?

Hapana, madaktari mlioaminiwa na chama mmefeli over confidence Ni mbaya sana. Kauli za Bashiru, Mwakyembe, Mhongo na wengineo wanaoamini Watanzania wanaishi kwa kuongozwa kwa wingi wa makaratasi ya CV mnaliteketeza Taifa.

Kuongoza watu siyo wingi wa vyeti ni wingi wa busara, hekima na intelligence ambavyo vyote hivi havisomewi unazaliwa navyo.

Tafuteni hoja, fungueni media ziripoti, ingieni mtaani tuwaambie wananchi tumefanya nn na tunataka tufanye nn then tuache wapige kura. Vyombo vya dola vinatulemaza, leo heshima ya PM inashushwa na Polisi huko jimboni kwake kwa Mambo yasiyoyamsingi. Hivi Waziri mkuu kweli Ni mtu wakuogopa wagombea shindani? Au mnamchafua na kumwaribia kesho yake kwa malengo mengine? Tujitafakari, wenzetu wanachanja mbuga bila hata msanii why not us
 
mziki, pool table na mpira wa simba na yanga wa kijinga
 
Nimependa sana .
umeongea kama mwanaharakati
Na sio mwanachama wa chama chochote.
 
Back
Top Bottom