Kwangu mimi huyu ndio kachero bora na mwana mikakati hodari zaidi ya Membe

Kwangu mimi huyu ndio kachero bora na mwana mikakati hodari zaidi ya Membe

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari za asubuhi ndugu zang wa JF,

Ama baada ya salam naomba nielekee sasa kwenye mada yangu. Ndugu zangu wakati nchi yetu inalazimishwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na nchi za magharibi, serikali ya Tanzania chini ya raisi wa wakati huo mzee Rukhsa ilikataa mfumo huu kwa kuona kwamba ni wa hatari na wenye lengo la kuitumbukiza nchi yetu katika machafuko ya kisiasa kama zilivyotumbukia baadhi ya nchi zilizokimbilia kukuubali mfumo huo.

Kwa vile wananchi (bila kujua faida au hasara ya mfumo huu) waliuhitaji, na kupitia mashinikizo mbali mbali kutoka kwa nchi hizo za magharibi including na baba wa Taifa mwalimu Nyerere, serikali haikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na mfumo huo kwa shingo upande. Lakini kabla ya kuukubali na kuupitisha mfumo huu serikali kupitia chama kilichokuwa kinatawala chini ya mwenyekiti wake mzee Ally Hassan Mwinyi, ilibidi wakae kwanza kikao cha dharura na faragha ili kuangalia namna watakavyo usimamia mfumo huo ili usije ukaleta madhara ya uvunjifu wa amani au vita katika nchi yetu.

Katika kikao hicho ndo ilipatikana idea au mawazo ya kuwa na watu wa mfumo ambao watakuwa wanapenyezwa kimya kimya katika vyama vya upinzani na hata tawala ili kujua mienendo na malengo ya vyama vyao hasa katika swala la amani, maendeleo na mshikamano wa Taifa letu lkn pia kuvuta mpunga kutoka katika nchi hizo za magharibi ili zisaidie kujenga shule, barabara, hospital nk. Baada ya kukubaliana na wazo hilo ndipo serikali ilipoukubali mfumo huo, na kuruhusu vyama vingi kuanzishwa kwa lengo la kuleta demokrasia, lkn yenye faida na manufaa ndan ya nchi.

Vyama vilipoanzishwa wazee wa kazi wakaingizwa kazini kusimamia kile walichoambiwa. Mwaka 95 NCCR kilikuwa juu sana lkn hakikuonesha sura ya kitaifa, kwahiyo wazee wa kazi wakaingia kazini na matokeo yake watu wakapigana viti katika mkutano wao wenyewe na kupelekea aliekuwa mwenyekiti wa chama hicho mh Augustino Mrema kuhamia chama kingine, na hapo ndio ukawa mwisho wa NCCR. Mwaka 2000 mpaka 2005 CUF ndio kilikuwa chama kikuu cha upinzani lkn macho kama kilivyokuwa NCCR, hakikuonesha kukomaa kupewa serikali hasa baada ya kugundulika kuwa chama hicho kina ukaribu zaidi na dini, wazee wa kazi wakaingia kazini chama hicho kikawa cha historia tu mpaka leo.

Baada ya hivyo vyama kuanguka, kikaja Chadema ambacho nacho hakikuonesha sura ya utaifa na kibaya zaidi kilijionesha kwamba kinaweza kupambana hata na serikali pale kinapohisi kuonewa. Chama hichi kilikuwa na vijana wengi ambao wengi wao hawakuonesha kujali chochote kuhusu amani ya nchi. Kilifanya maandamano mbali mbali, kilipambana na dola na kuzusha tuhuma mbali mbali ambazo zingine zilikuwa za kweli na zingine za uongo. Baada ya mwenendo huo uliotishia amani na usalama wa nchi, mwaka 2015 ndo wazee wa kazi wakaingizwa tena kazini ili kuangamiza na kumaliza kabisa fyoko fyoko zao. Na kwa vile chama hicho kilikuwa na mchanganyiko wa wasomi na wasio wasomi basi ilibidi serikali ije na mbinu za kisomi kwa kutengeneza mazingira yakayowaingiza mkenge walengwa wao.

Mbinu hizi zilihitaji pesa na ugomvi wa hapa na pale ili kurahisisha kazi. Na kweli ugomvi ukatengenezwa katika ya mwenyekiti wa chama tawala na mkuu wa nchi wa enzi hizo dhidi ya swahiba wake wa miaka mingi. Na kweli mbinu hiyo pamoja na pesa iliyotaarishwa na wenye mipango iliwezesha kuwaingiza kingi viongozi wa upinzani ambao waliweka mbele tamaa ya pesa, na uroho wa kushika madara. Katika hilo wazee wa kazi walifanikiwa kuisambaratisha ngome iliyokuwa inaitwa UKAWA na kuwaacha vipande vipande wasioaminiana.

Yan Chadema haiamini NCCR na NCCR haiamini Chadema. Hapo hatujazungumzia madiwani, wabunge na zile nguvu walizokuwa nazo katika kukabiliana na vyombo vya dola. Mwaka 2020 anaeitwa kachero mbobezi na yeye alipewa test ndogo tu ya kukasambaratisha kachama kadogo na kenye umri mfupi toka kaanzishwe lkn cha kushangaza mbobezi alishindwa mapema sana kumalizia kazi na kibaya zaidi alishindwa hata kuondoka na mwenyekiti wa serikali za mitaa hata mmoja.

Tofauti na mwenzake ambae alifanikiwa kuusambaratisha umoja wa ukawa na pia aliondoka na mamia ya madiwani na wabunge huku akiwaacha wapinzani wenyewe wakishikana uchawi wasiaminiane hata wenyewe kwa wenyewe ndan ya vyama vyao. Hizi ndio siasa za Tanzania bwana kama huzijui unaweza kuingizwa chaka na wajinga wajinga.

images (29).jpeg

2878995_images_9.jpeg

images (30).jpeg

images (32).jpeg
 
ACT walimzidi kete na kumuweka benchi na mapema sana Membe ila nae alishtukizia kuwa ameshadukuliwa mipango yake ,ACT walimtenga vibaya sana akapanga mikakati na CCM aende nje ya nchi akirudi akamatwe pale airport, mipango yao ni kutaka kuanzisha fujo ACT wakapewa michapo, jamaa na mipango yao ikabuma. CCM wakaona maalim amewazidi na ndio ukaona membe hakupewa kipaumbele alichwa kama alivyo.
 
Yaani ambacho sielewi hadi sasa kwa nini huyu bingwa hakufanya mkutano hata mmoja baada ya kuteuliwa na ACT kugombea Urais? wabobezi njooni mtujibu.

Mana alivyokuwa anaulizwa anajibu - "kimya kingi...." Sasa huu wa jana ndiyo mshindo mkuu? yaani "The return of undertaker" au njaa tu kama njaa zingine?
 
Yaani ambacho sielewi hadi sasa kwa nini huyu bingwa hakufanya mkutano hata mmoja baada ya kuteuliwa na ACT kugombea Urais? wabobezi njooni mtujibu.

Mana alivyokuwa anaulizwa anajibu - "kimya kingi...." Sasa huu wa jana ndiyo mshindo mkuu? yaani "The return of undertaker" au njaa tu kama njaa zingine?
Mwisho wake ndiyo hivyo ameamua kupiga magoti kwa mzenji
 
Huyo jamaa ana roho mbaya shetani anasubiri.....alishindwa kuupata urais akiwa na influence kwenye chombo kile.....asahau kuupata milele......machozi ya kina wale lazima yaendelee kumuandama
 
Mi nadhani saa ingine mnajitukiza tu nahuo ukachero.

Ukweli nikua, LOWASSA Alikua anautaka kweli Urais wa CCM kwelikweli.

Ila baada ya kukaziwa na kusalitiwa akawa hana namna.

Nakwakua aliaminishwa na Yule Ex DG wa TISS + mabilion ya akina Ndomba, ...na kwa kuutuliza moyo wake, nakutaka kuwaonyesha CCM kua Yeye ananguvu ..

Akaamua kuja UKAWA ,jiwe walolikataa waashi, likawapa UKAWA wabunge wengiiiiiiiiii .

Vivo ivo kwa Membe, Membe naye Jeuri zake , kujimwambafai n.k, akatemwa na JPM
Ili nayeye sasa kutapatapa, akahamia ACT ...

Et kusambaritisha Chama?? Ivi ACT ina athari gan kwenye siasa za Tanzania , mpaka atumwe mtu kukiua???.

Mambo mengine mnayakuuuuuuuuuza kumbe yanahitaji simple logic tu.
Mkuu umetiiishaaaa sana
 
Mwenyewe anajiona bonge la mchambuzi kumbe kiazi tu,kwahiyo hao "wazee wa kazi" kwao nchi kuwa na amani lazima iwe chini ya CCM? Hakuna cha wazee wa kazi wala mavi, kwanza sio kweli hayo matukio yote ni ya kupangwa,pili hata kama yapo kweli matukio ya kupangwa miongoni mwa hayo uliyo yaorodhesha si kweli kwamba ilikuwa ni kupigania amani ya nchi bali ilikuwa ni kupigania madaraka kwa sababu ya ulafi wa CCM na yamefanyika hayo bila kujali mustakabali wa amani iliyopo.
 
Kula tano kwa kumpa majibu stahiki huyo kilaza mzee wa ccm.
Mwenyewe anajiona bonge la mchambuzi kumbe kiazi tu,kwahiyo hao "wazee wa kazi" kwao nchi kuwa na amani lazima iwe chini ya CCM? Hakuna cha wazee wa kazi wala mavi, kwanza sio kweli hayo matukio yote ni ya kupangwa,pili hata kama yapo kweli matukio ya kupangwa miongoni mwa hayo uliyo yaorodhesha si kweli kwamba ilikuwa ni kupigania amani ya nchi bali ilikuwa ni kupigania madaraka kwa sababu ya ulafi wa CCM na yamefanyika hayo bila kujali mustakabali wa amani iliyopo.
 
Yaani ambacho sielewi hadi sasa kwa nini huyu bingwa hakufanya mkutano hata mmoja baada ya kuteuliwa na ACT kugombea Urais? wabobezi njooni mtujibu.

Mana alivyokuwa anaulizwa anajibu - "kimya kingi...." Sasa huu wa jana ndiyo mshindo mkuu? yaani "The return of undertaker" au njaa tu kama njaa zingine?
Bingwa alikuwa kazini kama alivyokuwa Lowasa lkn huyu alishindwa kutumia uzoefu wake ku act. Ndo maana alishtukiwa mapema.
 
Mabere Nyaucho Marando wakili wa mchungaji Mtikila Rip!
Huyu ndio alikuwa think tank wa mwenyekiti wa Chadema na wakili mkubwa Chama. Kwahiyo kuja kwa Lowasa ilikuwa ni sawa na kukanyaga fanda la ndizi.
 
Back
Top Bottom