Kwani gari Toyota VX "Geita Model" ni bei gani dukani? Na taratibu za manunuzi serikalini zikoje?

Kwani gari Toyota VX "Geita Model" ni bei gani dukani? Na taratibu za manunuzi serikalini zikoje?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nilimsikia waziri wa fedha Dr Mpango akiwaambia watumishi wa Hazina kwamba fedha zinaliwa sana kwenye halmashauri kwa kutumia utaratibu wa sasa wa " Fosi Akaunti"

Jana nikamsikia waziri wa Tamisemi Jaffo akisema DED wa Geita alitumia mwanya wa kuvunjwa Baraza la Mawaziri akakimbia haraka haraka kujinunulia Toyota VX kwa bei ya kilanguzi.

Ndiposa nauliza:

1. Bei halali ya Toyota VX ni Tsh ngapi?

2. Utaratibu wa manunuzi serikalini ukoje?

3. Baraza la mawaziri lilivunjwa lini?

4." Fosi Akaunti" hutumiwa sana na Mh Jaffo kwenye ujenzi wa zahanati na shule, je tumepona kweli huko?

Tuchape kazi jamani sasa hakuna madiwani wa Chadema wa kuwasingizia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Bei inatofautiana mkuu kulingana na model. Kwa level ya DED Sheria haimruhusu kununua gari la namna hiyo hata JPM aliligusia, maoni yangu hyo gari nilivyoiona haifikii mil 400 gharama ipo exaggerated Sana.

Hata hvyo huyo DED wa Geita ni moja ya MADED washamba sijawah ona unapigwaje hela kishamba hivyo aiseee!
 
Bei inatofautiana mkuu kulingana na model, Kwa level ya DED Sheria haimruhusu kununua gari la namna hiyo hata JPM aliligusia, maoni yangu hyo gari nilivyoiona haifikii mil 400 gharama ipo exaggerated Sana.
Hata hvyo huyo DED wa Geita ni moja ya MADED washamba sijawah ona. Unapigwaje hela kishamba hvyo aiseee
Na utaratibu wa manunuzi ukoje?

Hakuna tenda?
 
Bei inatofautiana mkuu kulingana na model , Kwa level ya DED Sheria haimruhusu kununua gari la namna hiyo hata JPM aliligusia , maoni yangu hyo gari nilivyoiona haifikii mil 400 gharama ipo exaggerated Sana ....
Hata hvyo huyo DED wa Geita ni moja ya MADED washamba sijawah ona ....unapigwaje hela kishamba hvyo aiseee
We unadhani amepigwa hela?au amepiga hela?
 
Wamebaki Madiwani wa Kijani tutarajie Wataidhinisha ununuzi wa Land rover 109
Wamebaki Madiwani wa Kijani tutarajie Wataidhinisha ununuzi wa Land rover 109
Hivi wakati wa upigaji huo CDM walikuwepo?Ni rahisi kiasi gani madiwani wa CDM kupiga dili kwa mfumo wa mapato na matumizi ya halmashauri hapa Tanzania? CDM waliwahi kutawala nchi hii mwaka upi ili tuone tofauti na wale wa CCM?
Tusidanganyane,kwa hapa Tanzania kuna waliokula/wanaokula fedha za wanyonge kuliko CCM?
 
Na utaratibu wa manunuzi ukoje?

Hakuna tenda?
Utaratibu wa ununuzi wa Umma kuhusu kununua magari ni kwa kufuata mwongozo uliotolewa na Serikali ambapo baada ya Taasisi kupanga bajeti na kuweka katika mpango wa ununuzi kinachofuata ni kuomba kibali kwa Waziri mkuu na kikipatikana unaomba specifications kupitia TEMESA (Wizara husika). Baada ya hapo unaomba bei kutokana na specifications za gari kutoka GPSA. GPSA watatoa bei ambayo Taasisi inatakiwa kulipa ili kupata gari hilo.

Kuhusu bei nina imani ni sahihi kwa hilo gari, ila ni kubwa mno kwa watumiaji (DED). Lilipaswa labda liwe gari la Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Kulinunua kwa matumizi ya mkurugenzi ni ufujaji wa fedha za umma.

Hakuna tenda inayotangazwa kwani GPSA inanunua magari kwa ujumla (bulk procurement) hivyo upata discount na kuyauza kwa Taasisi za Serikali kwa bei chini ya market price. Utaratibu huo utumika kwa mafuta pia
 
Utaratibu wa ununuzi wa Umma kuhusu kununua magari ni kwa kufuata mwongozo uliotolewa na Serikali ambapo baada ya Taasisi kupanga bajeti na kuweka katika mpango wa ununuzi kinachofuata ni kuomba kibali kwa Waziri mkuu na kikipatikana unaomba specifications kupitia TEMESA (Wizara husika). Baada ya hapo unaomba bei kutokana na specifications za gari kutoka GPSA. GPSA watatoa bei ambayo Taasisi inatakiwa kulipa ili kupata gari hilo...
Nimekuelewa mkuu!
 
Nimekuelewa mkuu!
Nashukuru, nina uhakika hamna upigaji ila kuna ufujaji wa pesa. Mfano mtoto unampa elfu 10 asubuhi badala atumie elfu moja tu anatumia yote na ukimuuliza umefanya nini anakwambia nimenunua burger za Best Bites na soda ya kopo na milk shake. Mtoto anaweza kuwa amefanya vitu halali ila amefuja hela hajatumia kwa uangalifu kupata value for money
 
Utaratibu wa ununuzi wa Umma kuhusu kununua magari ni kwa kufuata mwongozo uliotolewa na Serikali ambapo baada ya Taasisi kupanga bajeti na kuweka katika mpango wa ununuzi kinachofuata ni kuomba kibali kwa Waziri mkuu na kikipatikana unaomba specifications kupitia TEMESA (Wizara husika). Baada ya hapo unaomba bei kutokana na specifications za gari kutoka GPSA. GPSA watatoa bei ambayo Taasisi inatakiwa kulipa ili kupata gari hilo.

Kuhusu bei nina imani ni sahihi kwa hilo gari, ila ni kubwa mno kwa watumiaji (DED). Lilipaswa labda liwe gari la Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Kulinunua kwa matumizi ya mkurugenzi ni ufujaji wa fedha za umma.

Hakuna tenda inayotangazwa kwani GPSA inanunua magari kwa ujumla (bulk procurement) hivyo upata discount na kuyauza kwa Taasisi za Serikali kwa bei chini ya market price. Utaratibu huo utumika kwa mafuta pia
Kupata kazi GPSA unapaswa kuwa na sifa zipi?
 
Back
Top Bottom