Kwani makampuni ya simu na BOT hamuioni hii fursa na kuitumia?

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Juzi nilienda NMB Bank ili kupata mkopo lakini nikashindwa kwa madai kuwa sina barua ya kuthibitishwa kazini (wakati huo nina salary slip 3, kitambulisho, barua ya utambulisho na vitu vingine). Zamani NMB Bank ukiwa na 'take home' hata ya laki 2 ungeweza kukopa hata milioni 7! Sasa hivi NMB mtu mwenye laki 3 'take home' anakopa mwisho Tshs Milioni 4, Poor NMB!

Nirudi kwenye mada; Kutokana na mshahara kuwa mdogo wafanyakazi wengi wa serikali wangependa kukopa kwa riba nafuu, nikajiuliza kama kwenye simu unaweza kukopeshwa 500 ukalipa shilingi 680, Je, si zaidi kama wangetoa mikopo mikubwa zaidi ya ile wanayochukua akina mcharo?

Natoa hoja.
 
Tatizo wabongo hatulipi mikopo, hizi benki sio wajinga.
Vigezo vya mikopo vinatokana na hali halisi ya jinsi watanzania wanavyolipa mikopo yao.
 
Tatizo wabongo hatulipi mikopo, hizi benki sio wajinga.
Vigezo vya mikopo vinatokana na hali halisi ya jinsi watanzania wanavyolipa mikopo yao.

mkuu Kang hujanielewa! kumbuka mkopo kwa mfanyakazi wa permenent terms halipi manualy bali anakatwa automatic kupitia chek namba yake! kama hawa airtel wanaweza kukopesha kwa udhamini wa laini yako tu je hii si zaidi?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Kang hujanielewa! kumbuka mkopo kwa mfanyakazi wa permenent terms halipi manualy bali anakatwa automatic kupitia chek namba yake! kama hawa airtel wanaweza kukopesha kwa udhamini wa laini yako tu je hii si zaidi?

Sawa unakatwa kwenye mshahara lakini mkopo unavyozidi kuwa mkubwa na wa kipindi kirefu ndo kuna chance kubwa ya kutolipa, kuacha kazi etc. Airtel wanakopesha kiasi gani?
 
Sawa unakatwa kwenye mshahara lakini mkopo unavyozidi kuwa mkubwa na wa kipindi kirefu ndo kuna chance kubwa ya kutolipa, kuacha kazi etc. Airtel wanakopesha kiasi gani?

mkuu unataka kukopa? hahahaha!
airtel wanaanza tsh 500 ukilipa utakopa tena tsh 1500 na kuendelea Kiukweli mcharo kawa mtamu ni uzushi tu.
 
Zamani gani hiyo ndugu ambayo ilikua ukiwa na take home ya laki 2 ungeweza kukopa 7 million? Hiyo zamani mie nilikuwa ni kibarua wa hii bank na tangu hapo NMB wanazingatia sana sheria ya BOT ambapo, mkopo unaopewa ni ule ambao installment yake (malipo ya mwezi) haitakiwi kuzidi moja ya tatu ya take home! So, kwa take home ya laki 2, installment haitakiwi kuzidi sh. 67,000 kwa mwezi na payment period kwa take home kama hiyo ni miezi 24... sasa piga hesabu za haraka haraka hapo uone hata kama hiyo 3 million ungepata!!!
 
Tatizo wabongo hatulipi mikopo, hizi benki sio wajinga.
Vigezo vya mikopo vinatokana na hali halisi ya jinsi watanzania wanavyolipa mikopo yao.
IN short hiyo sheria ya kumtaka mfanyakazi awe amethibitishwa ni kwamba anakuwa pensionable... hii pension ni security kwa bank endapo mfanyakazi anaacha kazi wakati kachukua loan!
 
Allan Clement, Jaribu pia kutembelea Equity bank napo naona watu walioserikalini wana conditions nafuu kidogo kuliko haya mabenk mengine, all the best..
 
mkuu unataka kukopa? hahahaha!
airtel wanaanza tsh 500 ukilipa utakopa tena tsh 1500 na kuendelea Kiukweli mcharo kawa mtamu ni uzushi tu.

Sasa mkopo wa 500 na wa mamilioni risk ni tofauti sana, hauwezi kufananisha hivi vitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…