Kwani Mbowe hawezi kuwa Gaidi? Sura ya gaidi inafananaje?

Kwani Mbowe hawezi kuwa Gaidi? Sura ya gaidi inafananaje?

Chee4

Member
Joined
May 17, 2021
Posts
35
Reaction score
125
Kumekuwa na nguvu kubwa sana kutoka ndani na nje ya nchi kuhusu kukumatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa tuhuma za ugaidi nchini Tanzania.

Vyombo vya habari vya nje mfano BBC, Aljazeera, VOA na vingine vingi na magazeti mbalimbali ya mtandaoni yamekuwa mstari wa mbele kulaumu kuwa Mbowe hawezi kuwa gaidi.

Sio hivyo tu wanaharakati wa nje na ndani ya nchi, baadhi ya serikali za mataifa mbalimbali kama Marekani na taasisi za haki za binadamu zimelalamika sana kuwa Mbowe kaonewa aachie mara moja na wakaenda mbali na kusema Mbowe sio gaidi na kuwa kukamatwa kwake kunarudisha ustawi wa demokrasia nchini nyuma.

Swali langu la msingi kwa makundi haya haya yote ni je gaidi ana sura gani au umbile gani kama Mbowe hawezi kuwa gaidi.

Marekani kwa mfano ituambie magaidi yaliyopiga ubalozi wa Tanzania na Kenya mwaka 1998 walikuwa na rangi gani au umbile gani?

Marekani ituambie pia magaidi yaliyopiga jengo la biashara duniani Septemba 2001 walikuwa na nywele na kope zinafananaje?

Marekani pia ituambie kwa uzoefu wake wa kupiga vita ugaidi katika mataifa mbalimbali duniani magaidi wanavaa nguo za rangi gani au wanapenda kutumia dawa gani ya mswaki ili kuwajua kwa harufu.

Haya mashirika ya haki za binadamu yatuambie kila siku yanapotoa matamko dhidi ya vitendo viovu vya kigaidi sehemu mbalimbali yanaona magaidi yamevaa saa au miwani ya rangi gani?

Hivi vyombo vya habari mfano Aljazeera vituambie kwa nini baadhi ya wafanyakazi wake walishikiriwa misri kwa tuhuma za ugaidi na kelele zao mbona zilikuwa hazitaji magaidi wana sura gani?

Kwa maswali haya na mengine ambayo yanaweza kuulizwa ili kujua gaidi ana sura gani ni dhairi kumtambua gaidi kwa macho bali kwa vitendo vyake.

Ni katika mstari huu huu wa matendo ya Mbowe Polisi Tanzania imesema Mbowe amefuatiliwa muda mrefu na uchunguzi umekamilika wa kuwa amekuwa akiendesha vitendo vya kigaidi nchini.

Kwa kuwa uchunguzi umekamilika mataifa ya nje sasa waache mahakama za Tanzania zifanye kazi yake kwani Tanzania ni nchi huru na mahakama zake ni huru.

Katika mtiririko huo mataifa ya nje, wanasiasa na mashirika ya binadamu yafunge midomo kwani Tanzania haiwezi kushuhudia tena vitendo vya kigaidi ambavyo vimeuza na kuua wananchi wasiokuwa na hatia vikiendelea.

Namalizia na swali nililoanza nalo gaidi ana sura gani? Basi kama huna jibu subiri kesi ya Mbowe ianze.
 
Huwa wanayo agenda ya wazi na malengo dhahiri kama walivyo wale maharamia wa kijani.
 
Gaidi huanza kwanza kwa kudhulumu Mafao mfano NSSF na KUWEKA TOZO ZA KINYONYAJI.
 
Mbowe ni mmoja ya watu wajanja wajanja wa nchi hii walionufaika na ujinga wa watanzania, JPM hajawahi kumkubali huyu jamaa sababu alikuwa anajua figisu zake, na alishamweka kwenye rada zake, ikatokea covid ikambeba before hajamshughulikia vizuri, msaidizi wa JPM anamalizia alipoishia bosi wake. Abubakar hafai kwa maendeleo ya taifa letu, watu wote wenye nia njema na nchi hii tuungane kumpinga Abubakar na wafuasi wake.
 
Back
Top Bottom