kwani ni lazima wote turundikane Dar es Salaam?

majogajo

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
317
Reaction score
44
jaman kila mtu akiweka uzi wa kuomba kuanzisha biashara wanajamvi watamshauri location achukue maeneo ya Dar, sasa je sisi watu wa mikoani ndani yaani mawilayani tuanzishe biashara gani huko?
 
zipo biasharaa nyiingi na kubwa za kufanya mikoani....
nyingi mno
kilimo,hospitality...entertainment na kadhalika
 
Tena nafikiria kuna opportunity nyingi mkoani/wilayani kuliko Dar es salaam na hasa ukiwa creative ukafanya kitu tofauti kidogo. Pia fikiria biashara ya kuchukua vitu Dar es salaam na kuvipeleka huko mkoani/wilayani kwako, unaweza ukawa msambazaji wa some items/products wilaya nzima... you will make money..
 
Hilo lilikuwa swali zuri kama ungewauliza mawaziri.
 
si kweli unayoyasema,kama ni mfuatiliaji wa jukwaa hili utagundua 60%+ tunaoperate vijijini, dar zipo familia tu
 
Kweli jamani, wampwapwa na sisi mwishoni tutakimbilia mjini sasa.
 
Kweli jamani, wampwapwa na sisi mwishoni tutakimbilia mjini sasa.

Vipi nikileta biashara ya machinjio italipa hapo Mpwapwa? Nilipita siku moja huko nikienda Kibakwe, nikaona kila familia ina machinjio yake, ndio maana tunarundikana Dar.
 
Vipi nikileta biashara ya machinjio italipa hapo Mpwapwa? Nilipita siku moja huko nikienda Kibakwe, nikaona kila familia ina machinjio yake, ndio maana tunarundikana Dar.

italipa malila. Mbona kkoo maduka kibao na kila siku yanaanzishwa mapya. Ngoja tufanye kautafiti.
 
zipo biasharaa nyiingi na kubwa za kufanya mikoani....
nyingi mno
kilimo,hospitality...entertainment na kadhalika

kaka hyo nilo highlit bado sana huku mikoani.
na ni biashara ambayo kamwe hutokosa wateja.
 
kaka hyo nilo highlit bado sana huku mikoani.
na ni biashara ambayo kamwe hutokosa wateja.

ukumbi kama dar live
ukiweka mkoa kama mwanza au arusha
utavuna pesa mpaka ukimbie
 
ngoja nijaribu enterment.......ila maeneo mazuri yalishanunuliwa na wakubwa na wakayaacha idle, ukiulizia unaambiwa usiguse. cjui ntafanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…