Mamshungulii
Senior Member
- May 3, 2023
- 175
- 88
KWANI SH. NGAPI?
Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua silaha; kwani silaha tuliyochagua ni hela. Tunataka kuondoa unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila hela mapinduzi yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Hela ndiyo msingi wa maendeleo. Bila hela hakuna maendeleo”! Hii ndiyo imani yetu sasa.
Viongozi wa dini mawazo yao ni kwenye hela. Malezi ni hela, serikalini, wanasiasa na watumishi, mawazo yao na matumaini yao ni kwenye hela. Viongozi wa wananchi na wananchi wenyewe katika Kila sekta , na makundi mengine ya wananchi, mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni Hela. Ni kama wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata hela tutaendelea, bila hela hatutaendelea”!
Mpango wetu wa maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi shabaha yake ni hela tu. Na silaha yetu tuliyotilia mkazo sana ni hela. Ni kama tumesema, “Katika miaka 30 ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya,miundombinu na ili kutimiza shabaha hizo tunatumia Shilingi trilioni 900,000,000”. Kama tumetaja na tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha kubwa katika mawazo yetu, ni HELA.
Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo kwa HELA
Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani? Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge huyo kwa HELA .
Kiongozi wa Wafanyakazi anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza mishahara na kujenga majumba bora kwa HELA.
Kiongozi wa mashule anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa wa HELA!
Kiongozi wa wakulima akitaja shida yoyote ya mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za mkulima kwa HELA. Mradi kila shida inayolikabili taifa letu wananchi tunawaza Hela, Hela,Hela!
Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya makadirio yake ya matumizi yaani fedha wanazohitaji mwaka huo kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya maendeleo.
Wizara zinapoleta makadirio yao ya matumizi huwa zinaamini kwamba hela zipo ila mchoyo ni Waziri wa Fedha na Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna hela. Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia Wizara ya Fedha kwa kupunguza Makadirio yao ya matumizi. Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali itimize mipango mbalimbali huwa nao wakiamini kwamba hela zipo ila mchoyo ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba Serikali haina hela. Na kusema kuwa Serikali haina hela maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana hela. Kiasi walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi. Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa hela tunataka Serikali itumie hela zaidi. Na kama Serikali haina hela zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
TUSITEGEMEE HELA PEKEE KULETA MAENDELEO
Ni jambo baya kuchagua hela kuwa ndiyo chombo chetu kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini. Ni vibaya, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni vibaya kwa sababu mbili. Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo. Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi hela zao kwa hiyari ili zisaidie Serikali kuondoa dhiki. Njia ya kuzipata hela za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania, matajiri na maskini, hatuwezi kupata hela za kutosha kutimiza mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo yaweza kutoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna Serikali ya Dunia nzima. Hela ambazo nchi zenye neema hutoa huwa kwa wema wao, hiyari yao au kwa manufaa yao wenyewe. Haiwezekani basi, tupate hela za kutosha kwa njia hiyo.
JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEO
Mipango inayotegemea hela inakwenda vizuri lakini kuna mingi ambayo imesimama na yamkini mingine haitatimizwa kwa sababu ya upungufu wa hela. Lakini kelele zetu bado ni kelele za hela. Juhudi yetu ya kutafuta hela inazidi kuongezeka! Sio kwamba tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi ndefu na zenye gharama kubwa za kwenda kutafuta hela za maendeleo yetu, itafaa kufunga safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya kuleta maendeleo kwa kila mtu. Hii maana yake siokwamba sasahivi hatutajali hela, wala hatutajenga viwanda au kufanya mipango yoyote ya maendeleo inayohitaji fedha. Wala sikusema kuwa tangu sasa hatutapokea wala kutafuta hela kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu.
Ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo, hela ni moja ya matunda ya juhudi hiyo. Viwanda vitakuja, na fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao katika kufanya kazi kwa maarifa.

Upvote
1