Kwanini 40, mwenye ufahamu tafadhali

Kwanini 40, mwenye ufahamu tafadhali

Ally Kanah

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Posts
1,479
Reaction score
388
Nuhu alitengeneza safina kwa muda wa miaka 40, mvua ya Garika ilinyesha siku 40, Waisrael walikaa utumwani Misri kwa miaka 40. Pia Waisrael walisafiri Nyikani kwa muda wa Miaka 40, mnara wa Babeli ulijengwa kwa miaka 40.

BWANA YESU KRISTO, alifunga kwa Siku 40, pia alipaa Mbinguni baada ya siku 40,Pasaka inaadhimishwa baada ya Siku 40. Hata watu wakifiwa, humaliza msiba kwa kuondoa matanga baada ya siku 40, pia watu husema za mwizi 40, hata mtoto hutolewa nje baada ya siku 40.

Wastani wa kufaulu University semister moja kwenda nyingine na mwaka mmoja kwenda mwaka mwingine wa masomo ni marks 40. Ili uruhusiwe kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi ufikishe umri wa miaka 40.

Mtume. SAW alipewa utume akiwa na miaka 40,

Hebu leo nipe jibu "kwa nini ni 40?"
 
Back
Top Bottom