Kwanini 99% ya wanaofuga nyoka na wanyama wengine wakali huishia kuuliwa nao?

Kwanini 99% ya wanaofuga nyoka na wanyama wengine wakali huishia kuuliwa nao?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Miaka mitatu nyuma nilishuhudia Mfuga Wanyama Mmoja maeneo ya Pwani akiuwawa (akipoteza) Maisha kwa Kuuliwa na Simba aliyekuwa akimfuga na waliyezoeana na Kushibana kabisa.

Hivyo hivyo zaidi ya mara Nne nimewahi Kusikia Watu Wanne tena Wataalam kabisa wa Kufuga Nyoka (Mijoka) na ambao wamezoeana nao kabisa Wakiuwawa (Wakiuliwa) kwa Kung"atwa nao vibaya.

Najua hapa JamiiForums kuna Wabobezi Wakubwa wa Masuala haya hivyo mtanisaidia katika Kunielimisha na hasa kujua nini huwa kipo nyuma ya hali hii?
 
Kuna mdude huwa hayafugiki na imezibitika kisayansi kutokana na matatizo ya kupoteza kumbukumbu

So mnaweza kaa ata mwaka ila ipo siku atakusahau na kukudhuru
 
Mnyama pori ni mnyama pori tu, na ndio maana wamewekwa porini, ata uwe umezoeana nae vipi, kuna siku tu ule upori wake unamrudia.
Kuna kisa cha kweli cha jamaa fulani zamani alikuwa anafuga nyati mmoja akamchanganya na kundi la ng'ombe wake, kwahiyo akawa akiwachunga pamoja , siku moja kama kawaida anawapeleka malishoni, ghafla nyati uporipori ukamrudia bwan, alichota watu hovyohovyo na kuwaumiza vibaya, before akuwahi kufanya hvyo alikuwa nyati mwema tu..
 
Back
Top Bottom