Nimeshangaa Sana Kampuni ya Airtel walichonifanyia aiseeh @airtel_tanzania Kuna watu wengi wanalalamika kuhusu kushindwa kufanya fidia juu ya kilichotokea Mwezi mmoja uliyopita.
Toka oktoba 29 mwaka huu 2025 mitandao mingi ilifungwa kutokana na Changamoto iliyotokea kipindi cha Uchaguzi lakini, wiki kadhaa zilizopita ,
Airtel walisema wataweza kurudisha vifurushi au bando ambazo watu walijiunga ila wakashindwa kuperuzi.
Mimi ni mmoja wapo lakini mpaka Leo hii wameshindwa kufidia mpaka tumenunua bando jingine mlichokifanya Airtel hatujakipenda kabisa na Jana mtandao ulikua mbovu balaa.
Siyo airtel tu hata tigo walikuwa wanakata pesa kwenye account bila maelezo yoyote na ukifwatilia wanasema wanarudisha mimi binafsi hawajawai nirudishia miamala yangu mpaka leo tokea tarehe 26 october