Kwanini ajali ya Chacha Wangwe na Lissu madereva wao wote hawakudhurika? ?

Kwanini ajali ya Chacha Wangwe na Lissu madereva wao wote hawakudhurika? ?

KAKADO

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2012
Posts
230
Reaction score
336
Tutakumbuka miaka kadhaa iliyopita,mwanasiasa machachari wa wakati ule chache wangwe,alipata ajali mbaya ya Gari wakati akitokea dodoma kwenye vikao vyakibunge,njiani akiwa na dereva wake,inasemekana walipata ajali mbaya mno hali iliyopelekea ndugu wangwe kupoteza maisha,gari iliharibika vibaya sana ila upande wa dereva kutoka salama bila mkwaruzo wowotee mwilini,hali hii ilileta sintofahamu miongoni mwa watanzania,ukizingatia wakati ule ndugu wange hakuwa na maelewano mazuri na viongozi waandamizi wa chadema taifa,hasa katika kinyang'anyiro cha uongozi wa juu wa chama hicho.

Miaka kadhaa baadae mwanasiasa machachari wa upinzani Tundu lisu anapatwa na msukosuko wa shambulizi za risasi 32 zote zikiwa zimelenga kuupata mwili wake,bahati nzuri risasi chache ndizo ziliupata mwili wake na nyingi kupita mbali ya mwili, hali ambayo kila mmoja anaona ukuu wa Mungu katika jambo hili,chakushangaza katika tukio hili,ambalo lilimuhusu mheshimiwa lisu na dereva wake ambao wote walikuwa sehemu moja katika gari dereva hakudhurika hata kwakukwaruzwa na risasi hili linawezekanaje ingali lisu alikuwa mita chache kutoka alipokaa dereva?

Mazingaumbwe haya na ajali ya chacha mbona hayatofautiani?? Maswali yakujiuliza kwanini dereva asiumie kwa namna yeyote??

Muda utaongea hakuna jambo lisilo na mwisho ilitokea kwa wangwe dereva katoka mzima huku wangwe kapoteza maisha,ikatokea kwa lisu kwa bahati nzuri katoka majeruhi huku dereva katoka mzima wa afya bila mkwaruzo naamini siku moja ukweli utajualikana.
 
Screenshot_2017-09-10-09-10-17.png
IMG_20170910_103125.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kudhurika ama kutodhurika si hoja ya msingi, Hoja ni kuwa kwa nini serikali hii ya Chama cha Mapinduzi haifanyi uchunguzi wa kina na kuwakamata wauaji hawa? Hatuwezi kuwashuku madereva kwa hisia ili hali vyombo vinavyopaswa kufahamu na kutupatia ukweli vipo. Tuvitake vyombo hivyo vikiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu vituambie ukweli wa matukio haya ambayo ni aibu kubwa kwa Taifa letu.
 
assassination is not accident. kuwa na akili hata za kuvukia road. halafu jiulize inawezekanaje. mpinxani Wa serikali afanye tukio bila ya serikali kumuumbua? akili zako unazijua wewe tu.
 
the main point hakuwa dereva pia mashambulizi yalikuwa upande mmoja(upande wa lisu) pia huenda na position aliyokuwa amekaa ilisaidia,chengine kutokana na upande wa mashambulizi lisu alikuwa tena kama cover kwa dereva.. sioni uhusika wa dereva kwani ndie aliemkataza lisu asishuke,pili laiti angelikuwa ni mmoja wao angelishindwa nini kummalizia ili mishe iwe succes.. maana kwa mitutu hiyo ni dhamira ya kuuwa si kujeruhi
 
Madereva hawakuwa walengwa.
We jamaa nikuulize swali?? Unaona faida gani kudukua/kuiba avatar yangu aisee...Yaani hii avatar nimeibadilisha kwa kuwa mtu mwingine aliniibia nimeweka na hii na wewe umeeiba unaweka kwako kirahisi tu??

Acha usanii mkuu, Kuna mamilioni ya picha (avatar) huko lakini unaona SAWA kutumia hii ya kwangu ambayo nimeweka na jina langu kabisa...

kiroho safi nakuomba ubadilishe hii avatar kwa maana mimo nitaonekana msanii na hata sifa mbaya huku jukwaani..

Hapa JF kila mtu ana avatar yake inayomtambulisha...nakuambia hivi kwa kuwa wewe ni mgeni na hata kama ni mwenyeji umefungua ID mpya hilo jambo unalofanya ni UZINGUAJI MKUU..

ACHA WIZI WA KUIBA AVATAR ZA WATU

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk
 
Tutakumbuka miaka kadhaa iliyopita,mwanasiasa machachari wa wakati ule chache wangwe,alipata ajali mbaya ya Gari wakati akitokea dodoma kwenye vikao vyakibunge,njiani akiwa na dereva wake,inasemekana walipata ajali mbaya mno hali iliyopelekea ndugu wangwe kupoteza maisha,gari iliharibika vibaya sana ila upande wa dereva kutoka salama bila mkwaruzo wowotee mwilini,hali hii ilileta sintofahamu miongoni mwa watanzania,ukizingatia wakati ule ndugu wange hakuwa na maelewano mazuri na viongozi waandamizi wa chadema taifa,hasa katika kinyang'anyiro cha uongozi wa juu wa chama hicho.

Miaka kadhaa baadae mwanasiasa machachari wa upinzani Tundu lisu anapatwa na msukosuko wa shambulizi za risasi 32 zote zikiwa zimelenga kuupata mwili wake,bahati nzuri risasi chache ndizo ziliupata mwili wake na nyingi kupita mbali ya mwili, hali ambayo kila mmoja anaona ukuu wa Mungu katika jambo hili,chakushangaza katika tukio hili,ambalo lilimuhusu mheshimiwa lisu na dereva wake ambao wote walikuwa sehemu moja katika gari dereva hakudhurika hata kwakukwaruzwa na risasi hili linawezekanaje ingali lisu alikuwa mita chache kutoka alipokaa dereva?? Mazingaumbwe haya na ajali ya chacha mbona hayatofautiani?? Maswali yakujiuliza kwanini dereva asiumie kwa namna yeyote??

Muda utaongea hakuna jambo lisilo na mwisho ilitokea kwa wangwe dereva katoka mzima huku wangwe kapoteza maisha,ikatokea kwa lisu kwa bahati nzuri katoka majeruhi huku dereva katoka mzima wa afya bila mkwaruzo naamini siku moja ukweli utajualikana.
watanzania wa Leo si wajana ...baada ya ajali ya wangwe, makamba alikutwa na laptop ya wangwe, aliipata wapi ndani ya dk 15 baada ya ajali? Kwanini hoja binafsi ya wangwe juu ya mgodi wa nyamongo ulizimwa... Tafakari ... Kupandikiza migogoro kwa wapinzani ni sehemu ya mikakati endelevu ya maadui wa upinzani tanzania
 
Wakati mingine ni miujiza tuu kwani siyo lazima ufe au uumie wakati ajali inapotokea
 
naposoma post kama hizi huwa najiuliza binafsi "assasination plot/assasination attempt ifanywe na CHADEMA, PoliCCM wasikomae na uchunguzi hadi kumkamata muuaji?". Hutokea nikasogea mbele kidogo kujiuliza kilofa "kama CHADEMA wameua au wamejaribu kuua eg Chacha Wangwe, Mwangosi, Mtikila, Saanane etc, je PoliCCM wanazidiwa ujanja,mbinu na maarifa na CHADEMA?". Huwa sipati wa kumuuliza haya maswali anipe majibu so naishia kutabasamu na kuendelea kugida Mbege yangu
 
Haya matukio huwa wakati mwingine yanaleta majibu yenye kustaajabisha......

Kitu kibaya ni kwamba watu wengi wameshahukumu na wameshaamini ni mtu fulani ndiye amefanya hilo tukio.....
 
We jamaa nikuulize swali?? Unaona faida gani kudukua/kuiba avatar yangu aisee...Yaani hii avatar nimeibadilisha kwa kuwa mtu mwingine aliniibia nimeweka na hii na wewe umeeiba unaweka kwako kirahisi tu??

Acha usanii mkuu, Kuna mamilioni ya picha (avatar) huko lakini unaona SAWA kutumia hii ya kwangu ambayo nimeweka na jina langu kabisa...

kiroho safi nakuomba ubadilishe hii avatar kwa maana mimo nitaonekana msanii na hata sifa mbaya huku jukwaani..

Hapa JF kila mtu ana avatar yake inayomtambulisha...nakuambia hivi kwa kuwa wewe ni mgeni na hata kama ni mwenyeji umefungua ID mpya hilo jambo unalofanya ni UZINGUAJI MKUU..

ACHA WIZI WA KUIBA AVATAR ZA WATU

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk
Huyo n mtu aliyejulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom