N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Hali ya upungufu mkubwa wa mvua imeshatukabili, maeneo mengi ya nchi yetu January hii ya 2022 yanashuhudia uhaba mkubwa wa mvua.
Jitihada zetu kama Tanzania kwenye upandaji na utunzaji miti bado sio za kiwango cha kuridhisha.
Uvunaji miti holela kwa ajili ya makaa na kuandaa mashamba mapya unatuondolea uoto maeneo mengi.
NINI TUFANYE
Ifanyike kampeni ya kitaifa ya upandaji miti kwa angalau miaka mitatu mfululizo kwa ushirikiano wa:-
Tupande miti angalau miti Milioni Tano kila Halmashauri kwa mwaka kwa mfululizo wa miaka mitatu ili tupate mvua. Hali ilivyo haitii moyo kabisa.
Aidha tuwezeshe uzalishaji mkaa wa kupikia kutoka teknolojia ya taka tuachane na makaa ya miti...kama italazimika iwe kwa vibali maalum kwa mapori yaliyotengwa na kwa masharti ya KATA MTI PANDA MTI.
Wizara ya Mazingira kwa ushirikiano na TAMISEMI ije na Kampeni ya kitaifa itakayosimamiwa kwa dhati kila kaya iwajibike kupanda miti michache na kuitunza.
Tusanuke hali si nzuri.

- Wananchi
- Serikali Kuu (Wizara ya mazingira)
- Local governments
- JKT