Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Nimesikia mahojiano ya simu yaliyofanywa kwenye kituo kimoja cha redio cha Wasafi kufuatia tetesi zinazoenea za Yanga kufungiwa usajili.
Ally Kamwe ameonekana kusikitishwa na uvumi huo na kuuita habari za uongo.
Lakini hoja aliyotumia kupinga tetesi ni kwamba taarifa hiyo haijatolewa na official website za FIFA bali ni watu tu wameandika.
Mtangazaji alipotaka kuhitimisha mahojiano kwa kumuuliza Ally Kamwe kama Yanga walikwisha mlipa Lucy Eymael, cha ajabu Ally Kamwe alipatwa na kigugumizi na kushindwa kujibu swali hilo .
Badala yake alisema ni swala la taasisi hivyo hawezi kujibu.
Mpaka hapa Ally Kamwe ameonesha uwalakini kwenye swala la uwezekano wa Yanga kulipa deni hilo.