Kwanini Alteza?

kinehe

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
205
Reaction score
198
Wadau naomba kujua why now dayz ukipitia mitandaon hasa watu wanaouza magari used bongo alteza nikama inatangazwa sana tatizo nin kwny hii gari,
 
Mkuu, Altezza na pacha wake IS200, IS300, RS200 na AS300 ni gari nzuri sana. Imekaa sports sana, na ililetwa miaka ile ya 1998 kushindana na BMW 3, especially E36 na E46.

Sasa watu walivyonunua hapa mjini, wengi inawasumbua Mafuta kutokana na foreni na barabara za hapa mjini.

Engine ya Altezza zipo 2.0 L 1G-FE I6 (AS200/IS 200), 2.0 L 3S-GE I4 (RS200), na 3.0 L 2JZ-GE I6 (AS300/IS 300)

Kwahiyo 2.0L kwa hapa mjini, sisi wa kipato cha kawaida ni shughuli. Maana utakuta hadi inaenda 8KM au 9KM kwa Lita kukiwa na heavy trafiki.

Ndio maana nyingi zinauzwa kwa bei za kawaida 8-10M.

Ukitaka kununua, kama mafuta sio tatizo ni gari nzuri sana.
 
Daah lkn Mkuu km 8-9 per litre ni reasonable kabisa. Hio iki shinda mtu ahamie kwenye vitz /starlet tu Mkuu
 
Kuna wengine wanakubali exchange hadi na gari zenye engine ndogo kama IST, Vitz, Corolla etc kwa Top Up kidogo au Key to Key only.
Daah ni kweli kabisa Mkuu, lkn wakishindwa running cost za altezza basi gari nyingine za class hio zitawashinda tu aisee.
 
Kwanini ung'ang'anie altezza wakati inakutesa...wakati vitz inakupa raha!?
Nafikiria wakati wa kuishi real life umefika,fake life ni very costful...
Mwenye ile picha ya Rais wa Russia Vladimir Putin akifuel gari yake please anaweza kushare hapa....wenzetu wapo kwy level ya juu sana ktk kuishi maisha yao
 
1 litre for 8-9 km ndo ishu? Mbona hio ni consumption ya kawaida tu wala si ya kucomplain!
Sikatai mkuu. Kwenye paperwork ni ya kawaida. Sasa katika daily usage ni tatizo kidogo. Kama unakaa Mbezi unafanya kazi Posta, kila siku 10,000 (5.5L) unatumia.

Hapo tumetoa mizunguko mingine yoyote, kwahiyo ukiongeza mizunguko tu hapo unatumia hadi 15,000 per day.

Kwa week ya siku 5 ni 75,000 na mwezi ni Tsh 300,000.'

Hapo tumetoa kabisa weekend, trip mbali na kazini.

Ukiwa kwenye mtandao utaona Altezza inakunywa 1L kwa KM10 ila in reality mh inazidi.
 
na vipi kuhusu durability, spares na ulaji wa mafuta kwa toyota surf old model navutiwa na hili gari la juu wadau japo wengine naona wanayauza kwa bei ndogo. msaada jamani
 
 

Kabla mtu hujananunua gari ni muhimu sana lazima utizame kama unaweza kulimudu. Mfano mtu ananunua range rover 2016 kisha anatembea vioo kafungua! kama mie mmiliki wa kampuni nampokonya na pesa zake namrudishia. Tatizo watu wanavaba sana katika kununua magari, wengine wanataka makubwa kisha hawayawezi. Mi natumia lexus is200 (Altezza but ni 6 cylinders) na silalamiki unywaji wa mafuta coz its my choice, wakati nanunua najua what i am getting into. The only time nnapolalamika kuhusu mafuta ni pale napoona consumption imebadilika from normal. Anyways 10,000 tsh naendesha for 56KM, ofcourse ni highway hio (toka town kwenda shamba) but in town driving nafikiri labda 7Km/L au 8Km......
 
Umeeleza vizuri sana
 
Nipo na ww mkuu nishatembezaga hyo mnnyama tezza miez 6 tu likauzwa coz per day wese la elfu 10 lazma hapo ni tabata kwenda posta sijui ka zinazid kilomita nane...

Ukiwa na gari za kuanzia cc 2000 afu unategemea mshahara wa laki 8 kwa mwez huna mishe zengine ni ufala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…