Arab League ilianzishwa kwa maono ya viongozi wa Egypt na Syria kipindi kile kwa lengo hasa la kuitetea Palestina na kujipanga dhidi ya Israel in worst scenario. Saudi Arabia ni wajeuri huwa wanajikuta ndio leading Arab country, hapo anaongezeka Qatar ambaye hamuungi sana mkono Saudi Arabia. Kwa hiyo muungano umekaa kinafiki na Waarabu wanafikiana mno wale.
Miaka ilipita Israel ikapigana nao kadhaa vita mbili, Iran na Iraq zikapigana, baadae Gulf war Iraq ikaivamia Kuwait na kuelekea Saudi Arabia. Baadae ikatokea Iraq war. Kwahiyo kupigana ni maisha yao hapo bado haijaongeza magaidi na ukosefu wa demokrasia.
Saudi Arabia ni Wasuni hawapendani na waasi wa Houthi pale Yemen ambao ni Washia wakiungwa mkono na Iran. Syria pale Assad hafungamani na upande ila Washia wanamuunga mkono zaidi. Kwahiyo kinachowatenganisha ni ubinafsi wao, unafiki na madhehebu tofauti. Pia influence ya nje inachangia na ujue Israel haitokaa itulie kuona Waarabu hawagombani wanaongea kauli moja