Kwanini askari wa Urusi waliondoka eneo muhimu la Kharkiv? Ukweli huu hapa namna Counter Offensive ilivyofanya kazi

Kwanini askari wa Urusi waliondoka eneo muhimu la Kharkiv? Ukweli huu hapa namna Counter Offensive ilivyofanya kazi

Six Stars

Member
Joined
Dec 8, 2021
Posts
14
Reaction score
102
Jibu Fupi:
Ukraine ilionyesha Urusi jinsi upotoshaji kwenye vita unavyofanya kazi licha ya kuwa urusi ni kinara wa upotoshaji.

Jibu refu zaidi:
Baada ya urusi kushindwa kuuteka mji mkuu wa ukraine na kurudi nyuma kufocus na eneo la Kaskazini, Miezi kadhaa iliyopita tuliskia ukraine kakomboa eneo kubwa kharkiv, vikosi vya Urusi vililazimika kuondoka kwa njia fulani kaskazini mwa Kharkiv na kurudi nyuma tena kwani vikosi vya Ukraine vilikuwa na nguvu sana katika eneo hilo. Ilisababisha hali ya kimkakati ifuatayo katika mkoa huo🙁maelezo kwenye picha)

main-qimg-f7ae58273e48455c3536c10a572a49e8.png

Urusi alibaki na eneo dogo kharkiv huo mstari mwekundu kwenye picha ambao ulikua njia ambayo vifaa vyote vya Urusi kwenda Izyum vilikuwa vikipitia.(Russia’s supplies and logistics to izyum)

Hapo awali Izyum ilikusudiwa kuwa kitovu kikuu cha kuzindua mashambulizi ya kaskazini kwenye eneo kubwa la kuzunguka Donetsk/Luhansk. Ingawa hili halikutokea kweli, licha ya juhudi za Warusi, bado lilikuwa kitovu kikuu kwenye mashambulizi ya kaskazini. Kurudi nyuma kidogo kwa warusi ilitosha kuweka moja ya safu zao za mbele chini ya mkazo kwani ndo ilikuwa ndani ya range ya makombora ya ukraine - lakini bado warusi walikuwa salama sababu walikua wengi. Hatari ya eneo hili ni kwamba ilikuwa inategemea sana daraja la Kupiansk kwa njia ya usambazaji wa vifaa vyao(supply line)- kama lingetekwa au kulipuliwa ingeweka shinikizo kali kwa vikosi vya Urusi - hatari kubwa.

Kitu kingine vita vya Sievierodonetsk na Lysychansk vilichukua muda mrefu zaidi kuliko vile vikosi vya Urusi vilivyotarajia, vikiwa na majeruhi wengi zaidi kuliko walivyotarajia, na hawakuweza kupata mafanikio huko Bakmut. Hii ilisababisha kiwango cha juu cha kudhoofika kwa upande wa Urusi na kuipa jeshi la Ukraine wakati muhimu wa kuwapa silaha na kuwafunza wanajeshi wake wengi wa kujitolea. Haijulikani ni kiasi gani cha wanajeshi wa ziada Ukraine inawapa mafunzo sasa lakini inawasaidia na wanazidi kuwa bora na wenye silaha. Sehemu kubwa ya wanajeshi hawa wanafunzwa nje ya Ukrainie.

Kitu kingine muhimu hapa ni hali ya Kherson ambayo inafanana sana na ya Izyum-Kharkiv safu ya mbele:
main-qimg-24048afa4c0d4765fcfe5eda4f4e0d4d.png

Huo Mto kwenye safu za nyuma za Urusi , ilikuwa muhimu zaidi kwa Ukraine kuchukua ingerahisisha kuanza kuadvance kwa nyuma.

Ukraine walitumia miezi kadhaa kujijenga hapa na walianzisha mashambulizi madogo madogo lakini walilenga zaidi kulenga njia za usambazaji za Urusi (hasa madaraja na ilizidi kuwa hivyo tangu wapate HIMARS na mifumo mingine ya makombora ya masafa marefu). pia ilikuwa kuwa ikifanya advance hapa, ingawa polepole na kuna uwezekano kwa kiwango cha juu cha kuwapunguza warusi . Hii ilisababisha Urusi kuhamisha idadi kubwa ya wanajeshi na vifaa hadi Kherson.

Mwishoni mwa Agosti na mwanzoni mwa Septemba Ukraine ilitangaza kuzindua shambulio lao la counter offensive huko Kherson - kwa kufanya kelele nyingi kila mtu ajue na kuweka vifaa vyingi ndani yake - lakini pia walikuwa wakiweka vifaa vyao kwa siri mbele ya Kharkiv pia. wakati counteroffensive inaanza ukraine Walikuwa wamejihami na vifaa vya magharibi walivyo navyo na ilikuwa wazi kwamba vikosi vya Urusi sasa vilikuwa vimezidiwa - kumbuka Urusi ilihamisha wanajeshi wake wengi na vifaa kwenda Kherson baada ya kuona wanaangamizwa kwa kasi pia wakijua counter offensive inaanzia kherson kama ukraine alivyotangaza kwa kelele nyingi kiufupi walikuwa wameingizwa mjini.

Hatua ya kwanza ilikuwa kutumia pengo lililopatikana katika mistari ya Urusi kupitia huo mto hapo juu na kuzunguka upande wa kaskazini wa Balakliia katika hatua iliyopangwa kuzunguka jiji hilo.
main-qimg-03d168e70c2559a9a3521147e368d5e7.png

Vikosi vya Urusi vilishughulikia kile kilichotokea na kuanza kurudi nyuma - wengine waliweza, wengine hawakuweza.
Hatua ililofuata ilikuwa rahisi sana - safu za ulinzi za Urusi hazikuwa imara sana kwa hivyo mara baada ya kuvunjwa kwa nguvu kidogo Waukraine waliweza kuvuka.

Na unaweza kukisia walielekea wapi?


main-qimg-01185d7f0b477295dff9a6d69729306c.png

main-qimg-5be88ad2d4ccd30a415649987be4a05b.jpg
main-qimg-ae584a152d628f9b1d16a7c07d0b9271.jpg


(wapendwa Pro-Putin, hapo juu ni chanzo kinachounga mkono Urusi kikionyesha wazi kikosi cha Urusi kikiwasili, na kujaribu kuleta utulivu kwenye mstari wa kaskazini wa Izium, ikionyesha wazi kuwa huku hakukuwa na tactical withdrawal)

Baada ya kuvunja safu ya urusi ukraine walielekea Kupiansk - mahali tulipotaja hapo awali kuwa hatarini sana. Haijulikani kama vikosi vya Ukrain vililipua daraja hilo ili kuzuia kurudi nyuma kwa Urusi au ikiwa vikosi vya Urusi vililipua kama ngao yakutosogelewa wakati wanarudi nyuma. Kwa vyovyote vile daraja liliharibiwa na ghafla njia za usambazaji(supply line) wa Urusi hadi Izyum zilikaribia kukatwa kabisa.

Kwa vikosi vya Urusi ilikuwa wakati wa kutelekeza silaha kukimbia au kuzingirwa na kwa hivyo wakaanza kurudi nyuma bila utaratibu maalumu mwenye kupanda baskeli, kujichanganya na rai n.k ili mradi kuokoa maisha yao na ndani ya siku chache mbele ilionekana kama hii:
main-qimg-541cd9b85dead446f5475fb704f66f2e.png


Ilikuwa ni hali mbaya kabisa kwa upande wa Urusi na imeiacha Ukraine katika nafasi yenye nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali na vikosi vya Urusi katika hali ngumu sana huku hata Luteni Jenerali akikamatwa.

Kufikia tarehe 12 Septemba mbele sasa ilionekana kama hivi:
main-qimg-2aed35cc2627069af6df38628928b0b0.png


Mbaya zaidi ni kwamba vikosi vya Urusi karibu na Kherson vinaanza kuhisi vibaya juu ya suala la rasilimali.

kwa ujumla, sababu ya jeshi la Urusi kurudi nyuma ni kwa sababu hawakuwa na chaguo. kitu ambacho hakijakaa sawa kwa siku zijazo za "operesheni maalum" yao.

Mpaka hapo ambao bado wanasema hii ilikuwa ni "tactical withdrawal" na kwamba Counter-offensive ni propaganda. Mnakosea kabisa. Kupiansk ilikuwa kitovu kikuu cha vifaa vya Kirusi kutoka Belgorod na Veluyski - vifaa vilivyopita huko havikuwa tu vya kusambaza izyum, lakini pia severodonetsk. "tactical withdrawal" ambayo inahusisha kupoteza vifaa na kitovu hicho kikuu cha usambazaji hufanya njia za usambazaji kwa safu za Urusi kwenye eneo hilo kuwa chini na kwaa shida zaidi - na kwavile njia zote zilizobaki za usambazaji kutoka kaskazini kwa sasa ziko ndani ya safu ya Silaha za ukraine kutoka kwenye nafasi inayoweza kutetewa:

main-qimg-c2995fee98807288f565da867de446a6.png

Huku shughuli za kuadvance zikitokea upande wa nyuma wa Urusi upande huu wa mbele ni hatarishi kwani Ukraine sasa ina option nyingi za kuchukua ikiwa inataka kukata njia za usambazaji hadi Sievierodonetsk.
main-qimg-d7a4e495e569277ccea5f1bb5e52eb5c.png


wakati kwa vikosi vya Urusi vinavyotaka kuchukua Donetsk Oblest yote sasa vina option chache sana za kutenga Sloviansk na Kramatorsk - na kiukweli wameipa Ukraine njia kubwa ya kusambaza vifaa kwa maeneo hayo hayo. kwasasa ni rahisi Ukraine kusambaza silaha kwa vikosi vinavyopigana kwenye eneo la Donbas.

Kwa hiyo kama hii ni tactical withdrawal - basi ni ya kijinga.
 
Safi sana, uchambuzi umeeleweka.

Sun Tzu kwenye art of war alisema kuwa war is fought on deception. Ile counter offensive ya Kherson iliyotangazwa sana ililenga kuwatoa kwenye reli Warusi, matokeo yake wakapeleka askari wengi huko wakaacha Kaskazini uelekeo wa Kharkiv pakiwa na ulinzi dhaifu.

Sasa hivi Ukraine, anahitaji ndege tu za maana kama F-16 aweze kupiga offensive ya Kherson.

Nadhani Ukraine haitaki kuvunja daraja kule Crimea ili kuwapa Warusi mlango wa kukimbilia, maana usipowapa mlango wa kukimbilia watapigana vita kali sana na watakufa askari wengi sana pande zote
 
Umechambua vizuri sana hasa katika eneo Hilo ambalo Russia aliweka mikakati ya kushinda vita mapema kupitia izyum...
Bado kuna malofa wanafikiri Russia atashinda vitaa hii
Mpaka uite wenzako malofa...wewe unafikiri hasira zako na mapenzi yako..UKRAINE au Urusi wanayahitaji....Haya mwerevu....Ukraine wameshinda na Urusi kashindwa....vipi kuna jipya...????
 
Safi sana, uchambuzi umeeleweka.

Sun Tzu kwenye art of war alisema kuwa war is fought on deception. Ile counter offensive ya Kherson iliyotangazwa sana ililenga kuwatoa kwenye reli Warusi, matokeo yake wakapeleka askari wengi huko wakaacha Kaskazini uelekeo wa Kharkiv pakiwa na ulinzi dhaifu.

Sasa hivi Ukraine, anahitaji ndege tu za maana kama F-16 aweze kupiga offensive ya Kherson.

Nadhani Ukraine haitaki kuvunja daraja kule Crimea ili kuwapa Warusi mlango wa kukimbilia, maana usipowapa mlango wa kukimbilia watapigana vita kali sana na watakufa askari wengi sana pande zote
Ukivunja daraja maana yake unakata supply line,
 
Mpaka uite wenzako malofa...wewe unafikiri hasira zako na mapenzi yako..UKRAINE au Urusi wanayahitaji....Haya mwerevu....Ukraine wameshinda na Urusi kashindwa....vipi kuna jipya...????
Nisamehe mkuu Kwa kutumia lugha Kali nimejiona ni mkosefu Kwa lugha yenye kuudhi....
Tupo pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom