Kwanini baadhi ya media za Tanzania hawampendi msanii Diamond?

ndege joni

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
682
Reaction score
1,108
Nashangaa Tanzania tulivyo. Hivi karibuni msanii wa mziki Diamond Platnumz ametwaa mataji kama mawili huko Marekani ambayo ni moja ya kuletea umaarufu nchi kimuziki pia kuonesha kuwa anaweza kwa mashabiki wa Muziki. Walikuwemo akina Kiba, darasa, n.k lakini hawakufanikiwa.

Cha ajabu hizi habari hazikutangazwa kivile na baadhi ya vyombo vya habari. Zaidi tuliangalia kwenye mitandao... media chache walitangaza kama minor... nikimaanisha inakuwa habari ya mwisho n.k.

Na Huyu kijana akipataga misukosuko ya kimahusiano watu wanashoboka kila kona ya Dunia. Akiwemo dada yao Mange Kimambi. Ndo zinakua habari kubwa kuliko za ushindi anaoupata. Why apost negatives za msanii na sio postives zake?

Tufikirie kuhusu hili. Tunamuhitaji yule jamaa kimuziki kuliko madhaifu yake kimahusiano. Tukiendekeza utimu wa mpinzani wake anayemtegemea mange kupata promo hatutafika mbali. Nampongeza sana mond.. pamoja na media nyingi kutomsapoti hakati tamaa.
 

Ulishawahi kupita Newsrooms zao zote za wakakuambia / wakakuthibitishia kwamba hawampendi Ndomo Dimonde wako Mkuu?
 
Ww ni mchochozi na mchonganishi mkubwa,hicho kikao cha kusema wanamchukia kilikalika wap,nani alikuwa msemaji mkuu na walikuambia kwa sababu zipi wanamchukia?..

~Nyimbo tunazo sikia kwenye redio na tv,picha za magazetin ni vyombo vya habari vya kuzimu??mfitini ni mbaya kuliko hata mchawi
 
Its obvious... inaonekana. Natazama sana taarifa mbalimbali za TVs hawakuwa na time na hiyo kitu. Hata ikitokea naona inakuwa kama "by the way"

Naomba kabla ya yote nipime tu uelewa wako ili nijue najadiliana na Mtu wa aina gani au napoteza tu muda wangu. Hivi unajua maana ya Media Mkuu? Una una uhakika wa 100% kwamba Media za Tanzania hazikumpa ' airtime ' ya kutosha Ndomo Dimonde wako? Nitashukuru ukinijibu ila nataka Kwanza uanze na kunijibu nini maana ya Media na types / aina zake. Tuanzie hapo Kwanza tafadhali.
 
Media za Tanzania zingekuwa hazimpend diamond asingekuwa hapo alipo, kuna tatizo sehemu rejea kauli ya mond aliyosema hategemei media ili yeye kuwa juu, lawama zako ni ujinga
 
Akiweza kukujibu hizi nondo unitag nije kucheka.
 
Watu HAWAPENDI sababu ya Kuwa kibaraka Wa Bashite si zaidi ya hapo
 
Akiweza kukujibu hizi nondo unitag nije kucheka.

Nashangaa mpaka sasa bado tu hajanijibu bila shaka labda anafanya Consultation kwa wenye ' Tasnia ' yao waweze kumsaidia kumfundisha ( kumfunda ) ili siku zingine ajue kwamba kabla ya ' Kukurupuka ' kuanzisha mada humu ajue kuwa kuna JF ina Watu ' Vichwa ' ambavyo vimeshindikana halafu vinajiamini mno upstairs.
 
Siku zote mabaya yananafasi kubwa sana ya kujadiliwa kuliko mazuri....


Fanya mazuri 100 watu kimya... Fanya baya moja... Hata asiyekujua atajifanya anakujua ili akuzungumzie...

Ndiyo maana hata wasanii wa nje wanatengenezaga ma-beef ya uongo ili watu wawaongelee na kuuza kazi zao...

Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…