Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
TANESCO zamani nguzo za umeme hizi za milingoti zilidumu hadi miaka 20 na kuendelea kwa sababu licha ya treatment ya kuchemsha kwenye dawa, ziada ilikuwa
1. Shimo la kusimikwa nguzo kulimiminwa zege
2. Baada ya kuisimamisha nguzo ilishindiliwa kwa zege
3. Nguzo zilidumu kipindi kirefu sana hata zaidi ya miaka kutokana uimarishaji wa shimo la kusimikwa nguzo.
Je siku hizi wanafanyeje?
1. Shimo likichimbwa hawaweki zege chini wala hawamwagii material ya kuzuia mchwa na moisture.
2. Hawashindilii kwa zege.
Nguzo za milingoti hutumiwa sana Ulaya, Marekani hadi Asia na hudumu kipindi kirefu zaidi si chini ya miaka 20 na kuendelea sababu base humiminwa zege na ikisimamishwa nguzo hushindiliwa kwa zege kali.
Hii huifanya nguzo kuwa imara sana, kutoshambuliwa na mchwa na wala kutoathirika kwa moisture.
Haya ndiyo matatizo mojawapo yanayoikumba TANESCO kwenye miundombinu yake, husababisha matatizo ya mara kwa mara kwenye miundombinu ya umeme, haya ya kusimikaji nguzo za umeme kwa ubora yapo ndani ya uwezo wa TANESCO wenyewe, wala haihitaji kuagiza vitendra kazi na vifaa kutoka Ulaya na Asia. Majembe tunayo, sululu tunazo, kokoto zipo tele mitaani na cement inazalishwa nchini, ni utashi tu wa kuamua ujenzi wa miundombinu bora.