Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna mengi hatuyajui na mengine tunafanya tu bila kuelewa athari zake, kubwa na ndogo. Ulishawahi kula kwa mfano nyama ya ngo'mbe hasa hizi za supermarket? Ambazo ni mahususi kwa ajili ya kufugwa ili baadae afanywe kitoweo?
Huyu hutunzwa vizuri kuanzia kuzaliwa mpaka kuchinjwa na hata anapochinjwa huchinjwa katika njia ambayo wala hatambui. Ni jambia moja tu tayari limeshatenganisha mwili na kichwa. Hana muda wa maumivu. Hakioni kifo. Hayaoni mateso. Hivyo hana muda wa ku-generate sumu.
Hawa ni tofauti kabisa na hawa wetu wa kienyeji. Ni mateso mwanzo mwisho. Kuanzia pale mikoani let's say Dodoma kupakiwa kwenye fuso kwa fosi. Kutembezwa mwendo mrefu wa masaa bila chakula bila maji bila sehemu ya kujiegesha. Jua lao, mvua yao, upepo wao, joto na baridi vyote vyao.
Atafikishwa kama ni Dar akiwa hoi kabisa na huku akiwa ameshatandikwa fimbo za kutosha. Akiwa Dar machinjioni atawekwa sehemu chafu isiyo na huduma muhimu akiwa kazingirwa na tope kinyesi na maji machafu. Muda wa kwenda kuchinjwa hupelekwa mzobemzobe na bakora za kutosha.
Akifikishwa ni ngwala kamba kisu. Kwa mlolongo huu wa matukio ya kikatili mpaka anakata roho nyama yake inakuwa imeshaharibika vibaya kwa sumu za kutosha. Ukiila ladha yake ni tofauti kabisa. Unaweza kumlaumu mpishi kumbe shida sio yeye